Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sadio Mane - mashuti 19, mabao 9

Supastaa wa Liverpool, Sadio Mane anatajwa kuwa mchezaji mwenye kiwango bora zaidi kwenye Ligi Kuu England kwa sasa. Hajafunga mara nyingi sana, lakini Mane amehusika pia kwenye kutoa asisti. Lakini, kitu kingine kinachovutia ni kwamba mabao yake tisa ameyafunga kutoka kwenye mashuti yake 19 yaliyolenga goli.
 
Marcus Rashford - mashuti 24, mabao 10

Kitu ambacho Manchester United imekuwa ikitambia msimu huu ni huduma ya mshambuliaji wa Marcus Rashford. Kwa namna fulani ndiye kinara wao wa mabao akiwa amefunga mara 10 kwenye Ligi Kuu na kuwa kwenye orodha ya wanaofukuzia Kiatu cha Dhahabu. Rashford amefunga idadi hiyo baada ya mashuti 24 golini.
 
Aubameyang - mashuti 17, mabao 11

Straika wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang ameonyesha kuwa ni moto wa kuotea mbali kwenye Ligi Kuu England msimu huu. Fowadi huyo amefunga mabao 11 kwenye ligi na kuwa mmoja wa vinara wanaofukuzia Kiatu cha Dhahabu, lakini Aubameyang ameonyesha kuwa moto akifunga kwa mashuti yake 17 tu yaliyolenga goli.
 
Tammy Abraham- mashuti 24, mabao 11

Chelsea imekuwa na msimu mzuri kiaina, shukrani kwa huduma bora kabisa ya mshambuliaji wake, Tammy Abraham. Fowadi huyo kinda ameonyesha uwezo mkubwa kwenye ligi ya msimu huu ambapo amefunga mabao 11 baada ya kupiga mashuti 24 yaliyolenga goli. Jumla Tammy amepiga mashuti 43.
 
Jamie Vardy - mashuti 28, mabao 16

Kwenye Ligi Kuu England, straika Jamie Vardy ndiye kinara wa mabao akiwa ametikisa nyavu mara 16 kuing’arisha Leicester City kwenye michuano hiyo. Vardy amefunga mabao hayo baada ya kupiga mashuti 28 yaliyolenga goli. Mashuti yake yote kwa ujumla ni 41.
 
Back
Top Bottom