Washindi siyo watu wa kulalamika na kulaumu vitu na watu. Kuna watu ambao wao kutwa kuchwa ni kulaumu na kulalamika, ooh! hii serikali, aah! hii kazi, ooh! hii familia, aah! huyu mume au mke n.k.
Mtu analaumu na kulalamikia watu na vitu akidhani kuwa kwa njia hiyo atatatua matatizo yanayomkabili. Ni hakika kuwa siku zitapita na matatizo yake yatazidi na atabaki katika hali hiyo hiyo ya kushindwa.
“Kama hutokata tamaa, utafanikiwa.”
Dan O'Brien
Pasipo shaka mwanamichezo mashuhuri Dan O’Brien alifahamu wazi kuwa iwapo mtu hatokata tamaa atafanikiwa katika kila jambo analolifanya. Kukata tamaa ni sumu ambayo imewakwamisha watu wengi.
Mtu anapokutana na changamoto na kukata tamaa na kuacha kufanya kile anachokifanya, ni wazi kuwa hatoweza kufikia malengo yake. Kila mara kumbuka kuwa safari ya mafanikio ina changamoto ambazo zinahitaji uvumilivu ili kuzivuka.
Tabia kubwa ya watu walioshindwa ni kuwafanya wengine washindwe kama wao au kuwafanya wafikiri kama watu walioshindwa badala ya kufikiri kama washindi.
Watu walioshindwa wana maneno mengi na matendo mengi ya kukufanya ufikiri kama wao ili ushindwe kuliko kushinda katika lile unalolifanya.