Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mabao mawili ndani ya dakika nne yametosha kuipa Chelsea ushindi wa mabao 2-1katika London derby dhidi ya Arsenal ikiwa ni kipigo cha kwanza kwa kocha Mikel Arteta kweny uwanja wa nyumbani akiwa bosi Gunners.
 
Pierre-Emerick Aubameyang alifunga bao lake la 13 katika Ligi Kuu England msimu huu akiunganisha kwa kichwa kizuri krosi ya Calum Chambers baada ya kona ya Mesut Ozil na kuamsha shangwe kwa mashabiki wa Arsenal kwenye Uwanja wa Emirates.
 
Katika derby imeshuhudia wachezaji tisa wakipewa kadi za njano, kabla ya Chelsea kusawazisha kupitia makossa ya kipa Arsenal, Bernd Leno aliyeshindwa kuokoa krosi ya Mason Mount na kutoa mwanya kwa Jorginho kufunga bao la kusawazisha dakika 83.
 
Chelsea ilipata bao la ushindi dakika 87, kupitia Tammy Abraham aliyekimbia na mpira kutoka kati ya uwanja na kupiga pasi kwa Willian ambaye naye akamrudishia Abraham aliyepiga shuti la chini kufunga bao hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…