Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Lakini, fowadi huyo Msenegali, Mane, 27, alisema hawawezi kuacha lile lililotokea msimu uliopita lijirudie msimu huu.
Liverpool mambo yao ni safi msimu huu wakiongoza ligi kwa tofauti ya pointi 13 huku wakiwaacha pointi 14 wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa msimu uliopita, Man City.
 
Tumejifunza kutokana na makosa ya msimu uliopita. Kile kilikuwa kipindi kigumu sana kwetu. Kwa sasa tunajaribu kufanya akili yetu iwe inafanya kazi muda wote,” alisema.
“Unapopoteza ubingwa wa ligi kwa staili ile inaumiza sana akili. Mpango wetu ni uleule, kushinda kitu fulani. Kuna mechi nyingi sana mbele, lakini bado hatujachoka. Hilo halijawahi kuwa tatizo kwetu. Nadhani tupo vizuri msimu huu kuliko ule uliopita.
 
Lazima ujitoe muhanga kama ulipatwa na kilichotupata. Na sasa yupo sambamba kwa mapambano hadi mwisho.”
Liverpool watakipiga na Wolves leo Jumapili, mechi ya 12 ndani ya siku 36 na Alhamisi iliyopita walishusha kipigo kizito kwa Leicester City walipowachapa 4-0 kwenye Ligi Kuu England.
 
PEP Guardiola amekiri kwamba Manchester City wasahau tu kuhusu kuwakamata Liverpool kwenye mbio za ubingwa na sasa mpango wao ni kupambana tu kuwaondoa Leicester City kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi.
 
Kichapo hicho kimewafanya mabingwa hao mara mbili mfululizo kwenye Ligi Kuu England kubaki kwenye nafasi ya tatu nyuma ya Leicester City na vinara wasiofungika, Liverpool, ambao wamewaacha pointi 14 na mechi mkononi.
 
Kocha Guardiola alisema kipigo kinauma sana kwa sababu kimewaacha kwenye wakati mgumu wakiwa na jambo moja tu kupambana kuwamo kwenye nafasi ya pili na kuona suala la kubeba ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo ni ngumu.
 
Guardiola, ambaye kikosi chake kitacheza dhidi ya Sheffield United leo Jumapili, alisema: “Ni kujidanganya umeachwa pointi 14 na bado unaifikiria Liverpool. Sasa tunawafikiria Leicester, tunahitaji kurudi kwenye nafasi ya pili.
 
Bado tupo kwenye nafasi ya tatu, nafahamu viwango vya timu yangu na hii ni hali tu inatokea. Misimu miwili iliyopita tulikuwa tukishinda sana mechi na kuwa kileleni. Kwa sasa tupo nyuma sana na tunapaswa kujiweka sawa kiakili kwa ajili ya mechi zijazo.”
 
Guardiola aliulizwa kama sasa anahamishia nguvu yake kwenye makombe mengine ya ndani na kusema: “Hapana, hatuwezi kuhamishia mkazo huko, kuacha huku kwa sababu msimu ujao tutakosa kwenye michuano ya Ulaya.”
 
Mchezo huo wa juzi Ijumaa, Raheem Sterling alifunga mara mbili, lakini mabao ya Adama Traore, Raul Jimenez na Matt Doherty yalitosha kuipa Wolves ushindi muhimu huku msimu huu wakibeba pointi zote sita mbele ya Man City kwa sababu waliwachapa nyumbani na ugenini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…