Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Liverpool kwenye mechi zao, VAR imehusika mara sita msimu huu, nne zikiwapendelea na mbili tu ndio zimekwenda dhidi yao. Manchester City kwa upande wao, VAR imehusika mara nne kwenye mechi zao, tatizo zikiwa dhidi yao.
 
Kwenye ligi hiyo, Brighton ndio waliopata zali zaidi la kubebwa sana na VAR, mara saba ilipohusika kwenye mechi zao, mbili tu ndizo zimekuwa kinyume, wakati Wolves wao wakiongoza kwa kuadhibiwa zaidi na VAR. Wababe hao wa Molineux hakuna hata tukio moja la VAR lililokwenda upande wao na kufaidika, lakini sita yote yamekuwa dhidi yao
 
Tottenham Hotspur nao mambo yao si haba. Bila ya VAR, wangekuwa kwenye nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu England si kama sasa wanavyosika nafasi ya sita na wangekuwa nyuma kwa pointi tano. Lakini, msimamo wa sasa unaonyesha tofauti kabisa, hasa kwa Liverpool.
 
Chelsea walidhani wamesawazisha bao la Trent Alexander-Arnold, wakati Cesar Azpilicueta alipofunga uwanjani Stamford Bridge, ile Septemba, lakini VAR ilikuja kulikataa bao hilo kwa sababu Mason Mount aliyehusika kwenye pasi ya mwisho, alikuwa ameotea.
 
Novemba Novemba, hakuna aliyekuwa ameona Dejan Lovren kuwa amesukumwa na Jordan Ayew kwenye mechi ya Crystal Palace na James Tomkins kufunga bao, ambalo VAR ilikuja kulikataa. Liverpool wakaja kushinda dakika za mwisho mechi hiyo.
 
Novemba Novemba, hakuna aliyekuwa ameona Dejan Lovren kuwa amesukumwa na Jordan Ayew kwenye mechi ya Crystal Palace na James Tomkins kufunga bao, ambalo VAR ilikuja kulikataa. Liverpool wakaja kushinda dakika za mwisho mechi hiyo.
 
Kisha likatokea tukio la Jumapili iliyopita huko Wolves. Liverpool waliondoka uwanjani na pointi tatu, VAR ikikaa upande wao kwenye matukio mawili. Kulikubali bao la Sadio Mane, lakini kulikataa bao la Pedro Neto, lililokuwa la kusawazisha kwa Wolves, kisa mfungaji amezidi vidole tu.
 
Bao lile la Mane, kabla halijafungwa Virgil van Dijk alionekana kuunawa mpira, lakini kwa mujibu wa sheria ya Ifab, kushika kwa beki huyo kunakuwa hakuna maana kwa sababu mpira umepita kwa wachezaji wawili mbele, Adam Lallana na Mane, aliyefunga.
 
Mwamuzi wa zamani wa Ligi Kuu England, Dermot Gallagher alielezea bao hilo na kusema: ”Kitu kinachotazamwa hapa, ‘Huyo mchezaji aliyefunga, Mane, ameshika mpira? Hapana. Mchezaji wa mwisho kugusa mpira, Lallana ameshika? Hapana’.
 
Hao ni wachezaji wawili waliohusika kwa karibu kwenye bao hilo, mfungaji na mtoa pasi, hivyo Van Dijk alikuwa mbali sana kwenye uhusika.”
Hasira ya Wolves ipo kwenye kukataliwa kwa bao lao la kusawazisha la Pedro Neto, kwamba kulikuwa na mtu kuotea. Hilo lilikuwa moja kati ya mabao yaliyokataliwa na VAR kwamba wachezaji wameonea katika mechi za wikiendi iliyopita.
 
Lilianzia lile bao la Dan Burn wa Brighton kwenye mechi ya Bournemouth, likafuatia bao la Wilfried Zaha wa Palace kwenye mechi dhidi ya Southampton. Kisha bao la Teemu Pukki wa Norwich kwenye sare dhidi ya Spurs na kumalizia bao la Lys Mousset wa Sheffield United katika mchezo dhidi ya Man City
 
Back
Top Bottom