Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

KISA CHA BABU NA MJUKUU; CHAKULA KWENYE FRIJI KINAPOA TU! Baba mmoja alienda mjini kwa mwanae, alikua anaumwa na alichoka sana, siku moja akiwa kalala kitandani alisikia mke wa mtoto wake akiongea na mjukuu wake wa kike. Mjukuu alikua akimuelezea kuhusu mchumba wake ambaye alikua anampiga kila siku, alikua anamnyanyasa na siku hiyo mchumbe wake alimpiga sana baada ya kumfumania na rafiki yake, binti alitaka kuondoka na kumuacha ndipo kijana aliamua kuomba msamaha na kumvalisha pete. Binti alichanganyikiwa kwani alikua anampenda lakini alishachoka kupigwa, ila alikua anatamani ndoa na kuvalishwa pete ilimaanisha ndoa. Babu alimsikia Mama wa binti akimuambia akubali kuolewa kwani atakuja kubadilika, alimuambia wanaume wanabadilika hivyo chamuhimu ni kuvumilia na kumbadilisha taratibu. Babu alikasirika lakini hakufanya chochote, kesho yake aliwaomba wenyeji wake kuwapikia. Wote walishangaa lakini aliwaambia anakaribia kufa hivyo anataka kuwapikia chakula kizuri sana. Bila hiyana walimruhusu, alipanga kupika wali, walimnunulia mchele mzuri wa kunukia, nyama ya kuku nakumuacha apike. Alipika na kuweka mezani, chakula kilikua kinaonekana kizuri lakini walipoanza kula kwanza kilijaa chumvi, mchele ulikua mbichi, mboga aliweka sukari, na alichanganya na mchanga katika mboga. Kila aliyejaribu kula alishindwa na kutema. Babu aliwaambia wasijali, alichukua kile chakula na kukiweka kwenye friji, kilikaa siku mbili akakitoa na kuweka tena mezani. Aliwaambia wale lakini walishindwa, alikichukua na kukirudishe tena kwenye friji, baada ya siku nyingine mbili alikitoa tena na watuwalishindwa kula. Alifanya hivyo kwa wiki mbili, watu walichoka, siku moja mwanae aliamua kumtolea uvivu alikitoa na kukimwaga ili wasile tena. Usiku wakati wa chakula Babu aliulizia chakula chake, Mwanae alimuambia amekimwaga kwakua hakifai kula. Wakitegemea kua atakasirika Babau alitabasamu, alimuita mjukuu wake wakike na kumuuliza kama kajifunza kitu lakini hakuelewa. Ndipo Babu alimuambia “Wiki mbili zilizopita nilikusikia unaongea na Mama yako, alikuambia kuwa mchumba wako ambaye anakupiga na kukudhalilisha atabadilika hivyo uruhusu akuoe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…