Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Vifaa vya kukaangia Ni ukweli kuwa katika vyakula vyako utahitaji kukaanga chakula hata mara moja. Ni muhimu kuwa na kikaango (Frying Pan), kikorogeo cha chuma chenye mshikio imara wa mbao au plastiki na chujio la bati lenye kuweza kuweka chakula kilichotoka kwenye mafuta moto. Hivi vitasaidia kufanya kazi kwa kuaanga samaki, nyama, chips na vingine vingi. Miko ya mbao Uwe unapika mboga, wali, ugali, mchuzi au chakula cha aina yeyote, mwiko ni muhimu. Sababu tunatumia sufuria za bati, inashauriwa kutumia mwiko wa mbao sababu hauchubui sufuria. Hivyo, nunua mwiko wako, chagua mwiko wa wali au mboga (ina kama kishimo, au unafanana na upawa) na mwiko wa ugali (Uko bapa, mahsusi kwa kusonga ugali). Ukiwa na miiko miwili inatosha, huitaji zaidi. Mifuko ya kuhifadhia chakula Kuhifadhi chakula ni muhimu. Kuna vyakula vingine hutakiwa kuandaliwa na kuhifadhiwa kabla ya kuliwa baada ya muda mrefu. Kuna vyakula vingine huliwa na kubaki, hivyo ni vizuri kuhifadhi kwa matumizi ya baadae. Vyovyote itakavyokuwa, mifuko ya kuhifadhia masalia ua chakula ni muhimu kuwa nayo. Inapunguza kazi ya kuosha vyombo au kukupunguzia idadi ya vyombo unavyotumia kwa kuhifadhia kwenye jokofu. Je wewe una vitu gani unavyodhani ni muhimu kuwa navyo jikoni kwako? Tudokeze, na upate kuongeza kwenye orodha hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…