Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

[emoji837]Baraza la Congress la Marekani laiandikia Ikulu ya Tanzania kuwa hawatasita kuichukulia hatua Tanzania kwa yanayoendelea nchini
IMG_20200109_071432.jpeg
IMG_20200109_071422.jpeg
IMG_20200109_071427.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
JINSI YA KUTENGENEZA ICE CREAM YA VANILLA NYUMBANI : Vipimo: Maziwa ya maji kikombe1 ½ Nestle cream kikombe1 ½ (zipo kibao madukani ) Sukari nusu kikombe Chumvi kiduchu Vanilla ya maji kijiko 1 chakula Namna ya kutengeneza : 1. Changanya mahitaji yote vizuri katika bakuli hadi sukari yote ipate kuyeyuka vizuri. (Unaweza tumia blender kama huna mashine ya kuchanganyia ) 2. Mimina katika container ya plastic funika vizuri kisha itie katika fridge kwa masaa 4 au hadi iwe baridi kabisa, koroga tena kisha tia katika freezer igande kwa muda wa masaa 5-8 au usiku kucha. ENJOY!! 😎😎 NB: Kama maziwa unatumia mabichi (fresh) hakikisha unachemsha kwanza na kuacha yapoe kabisa kisha utaendelea kuyatumia. -
 
CHOCOLATE POPSICLE/ LAMBALAMBA ZA CHOCOLATE INGREDIENTS Maziwa 4cups Cocoa Powder 3cups Sukari 3/4cup METHOD Tia Vote Kwa Sufuria Ya Kupika,then Chemsha Kwa Muda Dakika Kama 2 Hadi Sukari Iyayuke,tia Kwa Kopo Ya Lambalamba,tia Kwa Friza,popsicle Ni Tayari
 
KITCHEN TIP: leo nimekuletea hii mdau wangu, jinsi ya kutengeneza tomato sosi nyumbani. 1. Osha kisha menya nyanya zako 2. katakata vipande vidogo vidogo au saga kwa kutumia blenda 3. Bandika sufuria zito jikoni kisha mimina nyanya zako. Koroga mpaka maji yakauke na libaki rosti zito la nyanya. 4. Ongeza limao, chumvi na sukari, koroga kisha acha mchanganyiko wako upoe 5. Weka kwenye kikontena halafu hifadhi kwenye friji. 6. Tomato sosi yako itadumu bila kuharibika kwa muda wa miezi mitatu
 
Kitchen tips: Safisha mafuta uliyokwisha kaangia samaki kwa kuyachemsha mpaka yachemke kisha utumbukize kipande cha ndimu au limao na kisha utoe uchafu wote ambao utakuwa upo juu. Mafuta yakipoa yatakuwa meupe na hayatokuwa na harufu!
 
Kitchen Tips: Jinsi ya kuhifadhi Nazi kwa wale ambao hampendi kukuna kuna kila Siku √ Chukua Nazi zako za kutosha zikune √ Kisha chukua contena au vimfuko vidogo vidogo vya plastic funga kadri ujazo utakao √ Kisha hifadhi kwenye friza ambalo linaweza kugandisha √ Ukitaka kutumia unachukua Nazi yako kwenye mfuko au kikontena unaacha inayayuka kisha unachanganya maji ya uvugu vugu unachukua Brenda yako unasaga kisha unachuja Nazi yako N.B mie hupenda kusaga Nazi kwenye Brenda sababu tui linatoka ziito kama maziwa yaani shata shata Ukihifadhi nazi zako hata za wiki mbili haukai kwenye mbuzi tena Je wewe huwa unahifazije nazi kwa ajili ya matumizi ya muda mrefu?
 
BAADHI YA VIUNGO, MATUMIZI NA FAIDA ZAKE -> Kitunguu saumu (Garlic) Kitunguu saumu ni kiungo ambacho kimekuwa maarufu kwa matumizi mbalimbali. Vipo vitunguu saumu vya rangi nyeupe ambavyo mara nyingi huwa na tumba kubwa ambazo ni chache. Vingine ni vile vyenye rangi ya zambarau au pinki ambavyo huwa na tumba ndogo na nyingi. Vitunguu hivi vina ubora sawa. Kitunguu saumu hufaa katika matatizo mengi kama kusaidia kuzuia maambukizi yatokanayo katika utumbo, mapafu na sehemu za ukeni. Vilevile husaidia katika uyeyushwaji wa chakula, kuzuia kuharisha na pia hupunguza fangasi za kinywani, maambukizi katika koo na hata mkanda wa jeshi. Kitunguu saumu kinaweza kutumika katika mapishi ya chakula, chai au kinywaji chochote cha baridi au cha moto. Mtu anapotumia vitunguu saumu atumie kwa kiasi. Inashauriwa kutumia vitumba visivyozidi sita kwa siku hasa kama vitatumika vibichi . -
 
Tangawizi (Ginger) Tangawizi ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa tangawizi. Kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kikiwa kimekaushwa na kutengenezwa unga. Ta n g a w i z i inaweza kutumika katika vinywaji vilivyochemshwa. Pia huweza kuongezwa kwenye vinywaji vingine au kwenye chakula. Tangawizi husaidia kuongeza hamu ya kula, kupunguza kichefuchefu, kutapika, kuharisha, maumivu ya tumbo na gesi tumboni. Pia husaidia uyeyushwaji wa chakula tumboni. Vilevile husaidia wakati wa matatizo ya mafua au flu.
 
Iliki (Cardamom) Iliki ni mbegu zinazotokana na mmea wa iliki ambazo hutumika kama kiungo. Mbegu hizi huweza kusagwa au kutwangwa na kuongezwa kwenye chakula au katika vinywaji. Iliki ni nzuri katika kusaidia kupunguza maumivu, kichefuchefu au kutapika. Pia husaidia uyeyushwaji wa chakula na huongeza hamu ya kula
 
Mdalasini (Cinnamon) Mdalasini ni kiungo kinachotokana na magome ya mmea wa mdalasini. Kiungo hiki huweza kusagwa au kutumika bila kusagwa. Vilevile mdalasini huweza kuongezwa kwe n ye chakula au katika vinywaji vilivyochemshwa au baridi. Mdalasini huweza kusaidia kupunguza matatizo kama mafua au flu, vidonda vya kinywani na hata fangasi za ngozi. Vilevile kiungo hiki huongeza hamu ya kula, pia husaidia kupunguza baadhi ya matatizo katika mfumo wa chakula kama kichefuchefu, kutapika au kuharisha. Kinywaji kilichochemshwa chenye mchanganyiko wa mdalasini na tangawizi kinaweza kutuliza kikohoz
 
Giligilani (Coriander) Giligilani ni aina ya kiungo ambacho majani na mbegu zake huwez a kutumika kama kiungo katika mapishi ya vyakula mbalimbali kama nyama, supu au mchuzi. Kiungo hiki husaidia kuongeza hamu ya kula na kupunguza gesi tumboni. Pia husaidia kuzuia maambukizi ya bakteria na fangasi
 
Kotimiri (Parsley) Kotimiri ni aina ya mmea ambao majani yake na mbegu zake huweza kutumika kama kiungo katika vyakula. Majani ya kotimiri husaidia kupunguza msokoto wa tumbo ambao mara nyingi hausababishi kuharisha. Vilevile kiungo hiki huchochea vimeng' e n yo tumboni na hivyo kuongeza hali ya kuhisi njaa. Mbegu za kotimiri huweza kusaidia kuondoa maji ya ziada katika mwili. Kiungo hiki huweza kuongezwa katika chakula wakati wa kupika au wakati wa kula.
 
Back
Top Bottom