Numbisa
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 348,970
- 1,252,247
Karafuu (Cloves) Karafuu hutokana na mmea wa mkarafuu. Kiungo hiki huweza kutumika peke yake au kwa kuchanganya na viungo vingine. Kiungo hiki husaidia kuleta hamu ya kula na kuboresha uyeyushwaji wa chakula tumboni. Vilevile karafuu husaidia kupunguza kichefuchefu, kutapika na kuharisha. Ni nzuri ikitumiwa katika supu, mchuzi, juisi ya matunda yenye uvuguvugu au vinywaji vingine vilivyochemshwa