Manchester United ni moja kati ya vilabu viwili ambavyo vimezungumza na kiungo wa Birmingham City Jude Bellingham, 16 anayecheza kikosi cha vijana wa umri wa chini ya miaka 17. (Mirror)
Kiungo wa Aston Villa Jack Grealish ameibuka kuwa mchezaji anayesakwa sana na mabingwa watetezi wa EPL Manchester City huku mahasimu wao Manchester United wakionyesha nia kwa mchezaji huyo wa miaka 24.
Wakala wa beki wa kati wa Arsenal Shkodran Mustafi atafanya mazungumzo na Galatasaray kuhusu mchezaji huyo kuhamia kwenye klabu hiyo ya Uturuki. (Fotomac, via Express)
Mlinzi wa kikosi cha Watford Christian Kabasele, 28, anakodolewa macho na Arsenal, Manchester United, Newcastle United na West Ham. (Le10 Sport, via Star)
Crystal Palace na Lazio ziko zinanyatia kumsajili beki wa Manchester United Ashley Young, 34, huku mchezaji huyo akiwa amepata ofa ya mkataba wa miezi 18 kutoka Inter Milan. (Sun)
Mshambuliaji wa timu ya Tromso Bryan Fiabema, 16 atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Chelsea tangu marufuku dhidi yao kuondolewa. (VG, via Mirror)
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez atakutana na LA Galaxy kujadili uwezekano wake kuhamia ligi kuu ya Marekani MLS. Mshambuliaji huyo raia wa Mexico alijiunga na Sevilla akitokea West Ham mwezi Septemba. (Marca)
Mlinda mlango wa Burnley Joe Hart, 32, alipendekezwa kujiunga na AC Milan badala ya Asmir Begovic wa Bournemouth ili kuchukua nafasi ya Pepe Reina San Siro. (Sun)