Mkurugenzi mtendaji wa Atletico Madrid Maguel Angel Gil Marin, alikuwa jijini Paris kufanya mazungumzo na PSG kuhusu mshambuliaji wao Edinson Cavani, 32. (Marca)
Manchester City imeondoa uwezewekano wa mlinzi wake wa kati Muingereza John Stones, 25, kujiunga na miamba ya London Arsenal katika dirisha hili la usajili. (Manchester Evening News)
Chelsea haina uhakika wa kutoa paundi milioni 40 kumnunua mlinzi wake wa zamani Muholanzi Nathan Ake,24 na pia hawatamsajili mchezaji mwenzake wa Bournemouth raia wa Uingereza Callum Wilson, 27. (Sky Sports)
Mkurugenzi mtendaji wa klabu ya Manchester United Ed Woodward ameonekana akisafiri kuelekea Ufaransa kwa kutumia treni ya Eurostar, United inapania kumsajili kiungo wa Lile mfaransa Boubakary Soumare, 20. (Star)
Mlinzi wa Ranger raia wa Ireland ya Kaskazini Danny Finlayson, 18, na mlinzi wa kushoto wa Uskochi Matthew Shiels, 19, wanatarajiwa kupelekwa kwa mkopo katika klabu ya Marekani ya Orange County. (Daily Record)
Mshambuliaji wa Los Angeles FC Carlos Vela atamkaribisha mshambuliaji wa Sevilla Javier Hernandez , hata kama mchezaji huyo mwenye miaka 31 atacheza na wapinzani wao LA Galaxy. (ESPN)
Mlinda mlango raia wa Ufilipino Neil Etheridge, 29, hatokuwemo katika kikosi cha Cardiff City kitakachoumana na Carlisle katika mzunguko wa tatu wa kombe la FA huku tetesi za yeye kuhamia Westham zikiendelea kushika kasi.(Wales Online)
Mshambuliaji wa zamani Darren Bent ametaka kujumuishwa kwa mlinzi wa kushoto wa Manchester United Brandon Williams, 19 katika michuano Euro 2020. (Talksport)
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.