Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Klabu ya Inter Milan imeafikiana makubaliano binafsi na kiungo wa Denmark Christian Eriksen,27, ili wamsajili moja kwa moja lakini klabu yake ya Tottenham inaitaka Milan kuongeza dau lao mpaka Euro milioni 10. (Calciomercato - in Italian)
 
PSG imeitaka Atletico Madrid kupandisha dau lao la usajili ili kumnasa nyota wa Uruguay Edinson Cavani kutoka Euro mioni 10 mpaka 30. Mshambuliaji huyo anamaliza mkataba wake na PSG mwishoni mwa msimu huu. (Marca - in Spanish)
 
Tottenham na mahasimu wao Arsenal ni miongoni mwa vilabu vitano vya ligi ya Primia ambavyo vinamuwinda beki wa Getafe na timubya taifa ya Togo Djene Dakonam, 28. Tayari klabu ya Monaco ya Ufaransa imeshakataliwa maombi yao ya kumsajili. (Sun)
 
Barcelona wanakaribia kumsajili kiungo wa Brazil Matheus Fernandes, 21, kutoka klabu ya Palmeiras kwa dau la Euro milioni 7, lakini pia kuna uwezekano wa euro milioni 4 kuongezeka. (Mundo Deportivo - in Spanish)
 
Kocha wa zamani wa Chelsea na Tottenham Andre Villas-Boas amedokeza kuwa huenda akaondoka katika klabu ya Marseille baada ya Afisa Mkuu wa zamani wa West Ham na Sheffield Wednesday Paul Aldridge kuteuliwa kuwa 'mshauri maalum' wa klabu bila yeye kufahamishwa. (Le Parisien - in French)
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] duuh
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…