Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

2.22674823678011622E18.jpeg
 
Robert Lewandowski

Taifa: Poland

Klabu: Bayern Munich

Mabao: 464

Mechi: 715

Safari ya Lewandowski ilianzia katika klabu ya Znicz Pruszkow hapo alifunga mabao 37, katika mechi 63, kisha akaja Lech Poznan mabao 41, mechi 82, hizi timu zote mbili za kwao Poland, hivyo baada ya kuwasha moto wa kutosha kwao akaondoka na kutua Ujerumani akijiunga na Borussia Dortmund, huku alifunga mabao 103 katika mechi 187.
 
Luis Suarez

Taifa: Uruguay

Klabu: Barcelona

Mabao: 470

Mechi: 754

Suarez balaa alianza kulifanya kwao Uruguay katika klabu ya Nacional unaambiwa katika mechi 34 za timu hiyo alifunga mabao 12, Ulaya wakamuona akatua Groningen ya Uholanzi hapo alicheza mechi 37 tu na kufunga mabao 15.
 
Ajax wakakiona kipaji chake wakamsajili huku ndiko alianza kuwa tishio zaidi Ulaya kwa sababu katika mechi 158 akiwa Ajax alifunga mabao 111, fasta Liverpool wakamuwahi akacheza mechi 133 na kufunga mabao 82 akiwa Anfield, Barcelona wakamdaka huku nako katika mechi 269 amefunga mabao 191. Huku akifunga mabao 59 katika mechi 113 za timu ya taifa ya Uruguay, huku mabao mengine matano akifunga katika timu za vijana za nchi hiyo.
 
Zlatan Ibrahimovic

Taifa: Sweden

Klabu: AC Milan

Mabao: 537

Mechi: 918

Achana na utukutu wake kwa ufupi Ibrahimovic anajua, maisha yake ya soka yalianzia Malmo FF ya kwao Sweden, ambako alifunga mabao 18 katika mechi 47, kisha Ajax akafunga mabao 48 katika mechi 48, akatua Juventus huku alifunga mabao 48 katika mechi 110.
 
Inter Milan alifunga mabao 66 katika mechi 117, Barcelona mabao 22, mechi 46, Paris Saint Germain mabao 156 katika mechi 180, Manchester United mabao 29, mechi 53, LA Galaxy mechi 58 mabao 53, AC Milan katika vipindi viwili Mabao 57, mechi 88. Timu ya taifa ya Sweden, mabao 62 mechi 116, kwa upande wa timu za taifa za vijana mechi 11, mabao 7.
 
Lionel Messi

Taifa: Argentina

Klabu: Barcelona

Mabao: 690

Mechi: 901

Shughuli yake kubwa ameifanya Barcelona kuanzia mwaka 2003, alifunga mabao matano katika mechi 10 za Barca C, kisha mabao 6 mechi 22 za Barca B, halafu sasa balaa likaja kwenye kikosi cha wakubwa ambako amefunga mabao 620, katika mechi 708.
 
Cristiano Ronaldo

Taifa: Ureno

Klabu: Juventus

Mabao: 718

Mechi: 1028

Mnyama mwenyewe huyu alianzia Sporting Lisbon B, ambako alicheza mechi mbili bila kufunga, kupanda Sporting ya wakubwa akacheza mechi 31 akafunga mara tano, akaonwa na Manchester United katika mechi 292 akafunga mabao 118, kisha akaenda Real Madrid huku katika mechi 438 akafunga mabao 450.
 
Back
Top Bottom