Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

855004691_294159.jpeg


There are microorganisms living on the seafloor that reproduce only once every 10,000 years and have been alive for millions. These are likely the oldest living things on Earth.
 
ERIC Daniel Pierre Cantona aliwasili Old Trafford kola yake ya jezi ikiwa imesimama. Ilikuwa Novemba 1992 wakati baridi ikianza kutawala miili ya wanadamu Ulaya. Cantona akaipasha joto miili ya mashabiki wa Manchester United.
 
Ni yeye ndiye aliyekuwa mchezaji wachache zaidi katika mwanzo wa utawala wa Sir Alex Ferguson. Inasemwa, kama ambavyo Dennis Bergkamp alivyoweka msingi wa soka la kisasa Arsenal, basi ni hivyo hivyo kwa Cantona na United
 
#Careers&work Life Pro Tip:

-------------✯✯✯-----------------

At your work, try to be involved in the process of hiring new employees, even if your job is not directly related to HR or hiring. This interviewing experience from "the other side" will give you great behind-the-scenes experience for your own future interviews for other jobs.

-------------✯✯✯------------------
 
Baada ya kutwaa ubingwa England na Leeds mwaka 1992, Cantona akaenda kutwaa ubingwa wa England na United mwaka 1993 na hivyo kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Ligi Kuu ya England kutwaa mataji mawili ya England mfululizo akiwa na klabu mbili tofauti.
 
Sikia, licha ya kufanya alichokifanya, ilimchukua Cantona miaka minne kuwa nahodha wa Manchester United. Alipewa unahodha mwaka 1996. Nani alifuata? Roy Keane. Alitua United mwaka 1993 lakini akapewa unahodha mwaka 1997 baada ya Cantona kuondoka zake.
 
Nani alifuata baada ya Keane? Gary Neville. Aliifahamu klabu tangu utotoni. Alipopewa unahodha mwaka 2005 ilikuwa ni kama miaka 15 tangu aijue klabu. Aliyefuata baada ya Neville? Nemanja Vidic. Alipewa unahodha mwaka 2011. Ilikuwa ni miaka mitano tangu ahamie klabuni mwaka 2006.
 
Aliyefuata baada ya hapo? Wayne Rooney. Alipewa kitambaa mwaka 2014. Kabla ya hapo alihamia klabuni hapo mwaka 2004 akitokea Everton. Aliyefuata baada ya hapo? Michael Carrick. Alipewa kitambaa mwaka 2017 ikiwa ni miaka 10 tangu ahamie klabuni hapo mwaka 2007 akitokea Tottenham.
 
Aliyefuata baada hapo? Antonio Valencia. Sir Alex alimnunua mwaka 2009 kutoka Wigan Atheltic. Ilimchukua miaka tisa kwa Valencia kupewa kitambaa mwaka 2018. Mwaka jana kitambaa akapewa Ashley Young baada ya Valencia kuondoka. Young alitua klabuni mwaka 2011 akitokea Aston Villa. Na sasa tuna mchezaji anayeitwa Harry Jacob Maguire.
 
Vigezo vya unahodha mara nyingi huwa havieleweki. Linapokuja suala la timu ya taifa fasheni imekuwa kumchagua mchezaji staa zaidi kuwa nahodha katika timu. Lionel Messi, Mbwana Samatta, Cristiano Ronaldo, Victor Wanyama ni miongoni mwa mastaa ambao wamepewa unahodha katika vikosi vya timu zao za taifa kwa sababu ya ustaa.
 
Katika klabu wachezaji upewa kwa sababu tofauti. Inawezekana ni kwa mchezaji aliyedumu zaidi kikosini. Inawezekana mchezaji anayejituma zaidi uwanjani. Inawezekana mchezaji anayeongea na kuwapanga wenzake Zaidi uwanjani. Inawezekana mchezaji anayetoa maelekezo zaidi uwanjani. Inawezekana mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi uwanjani.
 
Lakini zaidi ni kwa mchezaji anayeijua zaidi klabu. Mchezaji anayefahamu miiko na tamaduni za klabu. Mchezaji mwenye ushawishi kwa wenzake. Ndio maana manahodha wote niliokuhesabia hapo juu walipewa unahodha baada ya kukaa klabuni kwa miaka mitano au zaidi.
 
Leo Maguire amepewa unahodha baada ya miezi minne tu na inaashiria anguko la United kwa ujumla. Kuna mambo mawili hapa. Kwanza kabisa baada ya kuondoka kwa Ashley Young inawezekana Ole Gunnar Solskjaer alijikuta ameishiwa machaguo. Wachezaji waliokaa klabuni muda mrefu viwango vyao haviaminiki
 
Back
Top Bottom