Vigezo vya unahodha mara nyingi huwa havieleweki. Linapokuja suala la timu ya taifa fasheni imekuwa kumchagua mchezaji staa zaidi kuwa nahodha katika timu. Lionel Messi, Mbwana Samatta, Cristiano Ronaldo, Victor Wanyama ni miongoni mwa mastaa ambao wamepewa unahodha katika vikosi vya timu zao za taifa kwa sababu ya ustaa.