Hata hivyo, ukosefu wa watu wenye sifa umesababisha Maguire awe nahodha. Nadhani Ole alikuna kichwa akaona bora ampe tu. Hata hivyo, Maguire hana kiwango kizuri. Amekuwa akifanya makosa mengi. Sio mzoefu klabuni. Lakini pia ni mchezaji ambaye yeye mwenyewe hana cha kuwafanya awafokee au awaongoze wenzake.