Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

IMG-20200202-WA0039.jpeg
 
Ni ajabu lakini ndio ukweli wenyewe. Binadamu ana viungo vingi sana lakini ngozi ndio kiungo kikubwa kuliko vyote. Hii inatokana na ukweli kuwa ngozi ya binadamu inakadiriwa kuwa na ukubwa wa futi za mraba 14 hadi 18 kulingana na umri, jinsia yake, urefu na uzito pia.
 
Wapo baadhi ya wanasayansi walikwenda mbali zaidi na kusema, ngozi hufikia futi za mraba 20 lakini baadaye walionekana hawako sahihi sana kwa kuwa japo ni kazi ngumu kumpima binadamu ukubwa wa ngozi bila kumchuna, lakini uhakika hupatikana kwa kumpima urefu, uzito, kujua umri wake na jinsi yake tu, japo likichukuliwa karatasi jepesi ila gumu na kumvirigishia mtu kwa kuligundisha kila sehemu ya mwili wake akiwa mtupu, basi karatasi hilo likitolewa, likakatwa vipande na kuunganishwa, hupatikana jibu la ukubwa wa ngozi yake kwa usahihi zaidi.
 
Unene wa ngozi huzidiana pia katika maeneo tofauti ya mwili wa binadamu kwa mfano, ngozi ya mgongoni ni nene zaidi ya iliyopo kifuani huku usoni kukiongoza kwa kuwa na ngozi nyembamba katika kope kuliko sehemu zote mwilini.
 
Bila kuwa na nguo hii, tungeonekana kama roboti maana viungo vingi vya mwili kama mifupa, mishipa na vinginevyo vingekuwa hadharani na tungekuwa tunafuka vitu vingi toka mwilini. Ukiachana na hilo, ngozi inafanya kazi nyingi sana kwa faida ya maisha ya binadamu.
 
Lakini ngozi pia hutoa msaada mkubwa wa kuupa ubongo taarifa za mambo yanayouathiri mwili kwa nje na pia, ngozi hutoa taarifa kwa madaktari kuhusu magonjwa anayougua binadamu kama malaria, ngozi inaposhika joto na maradhi mengine mengi.
 
Yote haya ngozi huyafanya kwa kuwa ngozi imetengenezwa katika sehemu kuu tatu ambazo ni ‘Epidermis’ ambayo ni ngozi ya nje tuionayo na kazi yake kubwa ni kuzalisha seli mpya tunazoziharibu, kuifanya ngozi isipoteze rangi na baadhi ya seli zake ni sehemu ya kinga ya mwili inayolinda maradhi.
 
Sehemu ya pili ya ngozi ni ile ya kati iitwayo ‘Dermis’, hii hufanya kazi nyingi zaidi ikiwa ni pamoja na kumfanya binadamu atokwe na jasho linalotengenezwa na ‘sweat glands’ kutokana na sumu za mwili na hulitoa kupitia mirija iitwayo ‘pores’ kuja nje ya mwili.
 
Dermis ni ngozi inayotunza mishipa ya fahamu ambayo humfanya mtu awe na hisia kwa kuwa mishipa hiyo hupeleka taarifa kwenye ubongo. Dermis pia hutengeneza nywele na vinyweleo, hutengeneza mafuta yanayolainisha mwili na pia husafirisha damu kwenda kwenye sehemu zote za ngozi mwilini.
 
Sehemu ya tatu ya ngozi ni ile ya ndani iitwayo ‘Subcutaneos fat’ ambayo ina tishu maalumu zinazo iunganisha ngozi na misuli pamoja na mifupa mwilini. Sehemu hii ndio inayokuwa na mishipa mikubwa ya damu inayotoka kwenye ngozi na kusambazwa sehemu nyingine za mwili huku ikirekebisha kiwango cha baridi, joto na maumivu ambayo binadamu huyasikia kutoka nje na ndani ya mwili.
 
Back
Top Bottom