Klabu ya Juventus inapanga kutenga paundi za Uingereza milioni 150 wakati wa kipindi cha majira ya joto kumnasa beki wa Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi, Virgil van Dijk mwenye umri wa miaka 28. (Sun).
Klabu ya FC Barcelona inaelekea kufikia makubaliano ya kumnasa winga wa timu ya taifa ya Brazil na klabu ya Chelsea, William mwenye umri wa miaka 31, ambaye mkataba wake unatamatika mwishoni mwa msimu huu. (Marca).
Meneja wa klabu ya Arsenal, Mikel Arteta amezuia uhamisho wa kiungo wa kimataifa wa Ujerumani Mesut Ozil mwenye umri wa miaka 31 kwenda kujiunga na klabu moja ya nchini Qatar mwezi Januari. (90min).
Meneja wa klabu ya Everton, Carlo Ancelotti ameionya klabu ya FC Barcelona kuwa inapoteza muda wake kwa kujaribu kuwasilisha ofa ya juu zaidi kumnasa mshambuliaji wake wa Kibrazil Richarlison mwenye umri wa miaka 22, wakati wa kipindi cha majira ya joto. (Star).
Klabu ya Manchester United imeongeza juhudi za kujaribu kumleta kwenye klabu hiyo beki anayekipiga na klabu ya Napoli, Kalidou Koulibaly mwenye umri wa miaka 28. (Mirror).
United pia inawania saini ya kiungo wa Leicester City na timu ya taifa ya Uingereza James Maddison mwenye umri wa miaka 23 na pia winga wa klabu ya Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Uingereza Jadon Sancho mwenye umri wa miaka 19 wakati wa kipindi cha majira ya joto. (Standard).
Mshambuliaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Ufaransa, Olivier Giroud mwenye umri wa miaka 33, ameonesha kuchukizwa baada ya klabu ya Italia ya Inter Milan kuondoa ofa yake kutaka kunasa saini yake. (RMC, via Mail).
Klabu za Manchester United na Chelsea zimeshindwa katika juhudi zao za kumsajili mshambuliaji wa PSG, Edinson Cavan, mwenye umri wa miaka 32, kutokana na ukweli kuwa mchezaji huyo amependa zaidi kwenda kujiunga na klabu za Hispania. (Mirror).
Mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Japan, Takumi Minamino mwenye umri wa miaka 25, amesema klabu kadhaa za Uingereza zilionesha nia ya kutaka kumsajili pamoja na klabu ya Bundesliga. (Star).
Kiungo Steven Bergwijn mwenye umri wa miaka 22 ambaye amejiunga na klabu ya Tottenham akitokea PSV Eindhoven kwa makubaliano ya dau la paundi milioni 27 siku ya Jumatano, amekataa bonasi ya paundi milioni 6 ili abakie katika klabu ya PSV. (Mirror).
Arsenal itahiyajika kulipa paundi za Uingereza milioni 8 kupatasa saini ya mchezaji na beki wa kimataifa wa Hispania aliye kwa mkopo, Pablo Mari mwenye umri wa miaka 26 na beki wa kushoto wa Kireno Cedric Soares mwenye umri wa miaka 28 ili kuwa wachezaji wake moja kwa moja. (Star).
Chelsea imekataa ofa ya lala salama ya wachezaji Dalian Yifang na mchambuliaji wa Venezuela Salomon Rindon mwenye umri wa miaka 30. (Sun, via Telegraph).
Juventus tayari imeanza maandalizi ya majira ya joto kupata saini ya kiungo wa kimataifa Sandro Tonali mwenye umri wa miaka 19 kutoka klabu ya Brescia pamoja na kiungo wa kimataifa wa Ufaransa anayekipiga katika klabu ya Manchester United Paul Pogba mwenye umri wa miaka 26. (Calciomercarto - in Italia).
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.