Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Husaidia kupumzisha ubongo.Kumkumbatia mtu unayemjali au kumpenda kunasaidia ubongo kuzalisha homoni inayojulikana kama OXYTOCIN ambayo huusaidia ubongo kufikia kiwango kikubwa cha kupumzika, pia homoni ya OXYTOCIN humsaidia mwanamke mwenye ujauzito kujifungua kwa usalama zaidi kwani hufanya mfumo wa uzazi kupanuka.
 
Husaidia mwili kupambana na magonjwaKwa mujibu wa tafiti mbalimbali watu wengi hasa wazee wanaokumbatiwa mara nyingi huwa na asilimia chache za kukumbwa na magonjwa kuliko wale ambao hawakumbatiwi, hivyo watu hushauriwa kukumbatia wazazi wao kwani hii itawasaidia miili yao kuzalisha kinga ya kupambana na magonjwa.
 
Kukumbatiana husaidia kupunguza maumivuMadaktari hushauri kuwakumbatia wagonjwa wetu kwani kitendo hicho kidogo kinasaidia ubongo kuachia homoni inayojulikana kama endorphinsambayo husaidia kufunga njia zote katika ubongo ambazo hutuma taarifa ya kuwepo kwa maumivu kwenye mwili.
 
Husaidia watu kuwa na mood nzuriKwa mujibu wa tafiti mbalimbali watu wenye hasira au mood mbaya kila siku huzalisha homoni chache sana za Dopamine na Serotonin ambazo zinasaidia kufanya ubongo kuwa na uchovu na kukosa furaha hivyo kumkumbatia mtu unayempenda inasaidia kuzalisha homoni hizi kwa wingi.
 
Kukumbatiana huongeza ufahamu kwenye ubongoWatu wanashauriwa kuwakumbatia watu wenye uzito wa kuelewa mambo kwa haraka hasa wagonjwa wanaosumbuliwa na magonjwa kama Autismna Dementia kwani kitendo hiki husaidia ubongo kuzalisha homoni yaoxytin inayosaidia ubongo kuelewa jambo kwa haraka na kutatua maswali magumu.
 
Hupunguza msongo wa mawazoKukumbatiana kunasaidia kupunguza uzalishaji wa homoni inayoitwaCortiso ambayo husaidia ubongo ku-relax. Homoni hii ikizalishwa kwa wingi kwenye ubongo wa binadamu husababisha hutawaliwa na mawazo hasi yanayopelekea msongo wa mawazo.
 
Hupunguza msongo wa mawazoKukumbatiana kunasaidia kupunguza uzalishaji wa homoni inayoitwaCortiso ambayo husaidia ubongo ku-relax. Homoni hii ikizalishwa kwa wingi kwenye ubongo wa binadamu husababisha hutawaliwa na mawazo hasi yanayopelekea msongo wa mawazo.
 
Humsaidia mtu kupunguza hofuTafiti iliyofanywa na Psychological Science Journal imeeleza umuhimu wa kumkumbatia mtu mwenye hofu kwani inasaidia ubongo kupuuza taarifa hasi zinazotumwa kwenye ubongo pia husaidia mtu kuzalisha homoni zitakazomfanya ajiamini.
 
Huepusha mtu kupata magonjwa ya akiliKukumbatiana kunasaidia kuzalisha kwa wingi homoni ya Dopamineambapo uzalishwaji wa homoni hii husaidia ubongo kupambana na magonjwa ya akili kama Depression, Bipolar pamoja na Dementia pia homoni hii inasaidia mtu kujiamini na kuwa mkweli.
 
Husaidia kuepusha magonjwa ya moyoUtafiti uliofanywa North Carolina umesema kuwa watu ambao hawajaonana na wapenzi wao kwa muda mrefu mapigo ya moyo huongezeka kwa mapigo 90 kwa dakika ambapo hali hii sio nzuri kwani binadamu mwenye afya imara hupata mapigo 40 kwa dakika moja
 
Husaidia kupumzisha misuli ya mwiliKukumbatiana kunasaidia kupumzisha misuli ya mwili ambapo watu wengi wanapokumbatiana hulegeza misuli yote iliyokaza na kusaidia mwili kupumzika. Hii ndiyo maana wazazi wengi hushauriwa kuwakumbatia watoto wao wanapoamka asubuhi na kabla hawajalala
 
Katika enzi za mababu zetu, watu walikuwa wanaishi kwa raha, amani na upendo japokuwa walikuwa wanachagulia wake au waume wa kuishi pamoja kama mke na mume, enzi hizo zimepitwa na wakati siku hizi watu wanajitafutia wenza wao wenyewe, ila siku hizi watu ndio hawana amani, ndoa zinavunjika kila siku na wanaobakia kuteseka zaidi ni watoto ambao wanaishia kuishi bila mama na baba.
 
Ukweli ni kwamba inachukua muda mrefu kumfahamu mtu vizuri, kikubwa zaidi watu wanabadilika jinsi wanavyokuwa, hela zinaongezeka au kupungua na wanajikuta wanavutiwa na watu wa aina tofauti. Kwa wale ambao hawajabahatika kupata wenza wao kuna mambo ya msingi ya kuzingatia kabla hujajizamisha katika dimbwi la mapenzi, ukizingatia mambo haya, hata kama mtu uliyenaye atabadilika , uwezekano wa kuvumiliana na kuweza kuishi pamoja ni mkubwa zaidi.
 
1. ni lengo (ambition),

kama mmoja kati wa wapenzi (nazungumzia wapenzi ambao wanampango wa kuishi pamoja kama mke na mume) ni mtu wa kuwa na malengo na anataka kufanya kitu fulani au kuwa mtu fulani katika maisha yake na mwenzake anachukulia siku kama inavyokuja (laid back), huyu ambaye ana malengo atamchukulia ambaye ni “laid back” kama ni mvivu. Wapenzi wanatakiwa wasipishane sana katika malengo yao hata kama wana kazi mbali mbali.
 
3. wapenzi wanaweza kuwa tofauti katika ujuzi wa hisia (emotional intelligence).
Hapa kama tofauti sio kubwa, watu wanaweza kuvumiliana na kuishi pamoja, ila kama tofauti ni kubwa sana, yule ambaye hana ujuzi wa hisia, atakuwa anamburuza na kumharibia mudi yule ambaye amesimama imara kwenye mambo ya hisia. Onyo kwa wanaume ambao wana ujuzi au utaalam wa kusoma hisia za wanawake, wanawake ambao wana F katika ujuzi wa hisia huwa wanavutiwa sana na watu kama ninyi.
 
4. ni usosho,
kama mmoja wenu ni mtu wa watu anapenda kuongea na watu na anamarafiki kibao, utamkwaza ambae ni mtu ambaye anapenda maisha “private” na ya utulivu. Mwenzako atakuwa bize anaweka picha zenu na status zinazowahusu facebook wakati wewe unataka mambo ya ndani yawe ya ndani tu. Kama tofauti si kubwa sana mnaweza vumiliana kama tofauti ni kubwa, muda si mrefu mtashindwana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…