Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

FB_IMG_1580834613206.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Teh teh teh teh,[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] kuna habari hapa, kwamba una hatari ya kulea mimba lakini mtoto akatwaliwa na Ustaadhi aka Ostadhi[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089]

Sent using Jamii Forums mobile app
😄😄😄 yapuuze hayo maneno bro hayana ukweli wowote

#niWivuTu
 
Jumamosi iliyopita, chama hilo linalonolewa na Mjerumani Jurgen Klopp liliichapa Southampton 4-0 uwanjani Anfield na kuwafanya kufikia ushindi wa mechi 20 mfululizo za ligi wakishinda ndani ya uwanja huo, wakifukuzia rekodi yao ya miaka 48 iliyopita.
 
Jambo jingine ni kwamba Liverpool hawajapoteza mchezo wowote wa Ligi Kuu kwa mechi 42 zilizopita na hivyo kufukuzia rekodi ya mechi 49 bila ya kupoteza iliyoweka Arsenal 2005. Liverpool wao baada ya kukosa ubingwa msimu uliopita, kocha Klopp na wachezaji wake wamekuja kwa hasira kubwa msimu huu na kushinda mechi 24 kati ya 25 ilizocheza kwenye ligi hiyo hadi sasa, huku mechi pekee ambayo hawakushinda ilikuwa ya sare ya 1-1 dhidi ya Manchester United uwanjanni Old Trafford siku za mwanzo mwanzo za msimu.
 
Man City kwenye nafasi ya pili ndiyo timu ambayo ilikuwa ikishikilia ubingwa wa Liverpool kimtindo, lakini baada ya kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Tottenham Hotspur juzi Jumapili zinampa unafuu kocha Klopp na sasa kama atashinda mechi sita tu zijazo, anamaliza ukame wa miaka 30 wa Liverpool kubeba ubingwa wa Ligi Kuu England wakinyakua taji lao la kwanza
 
Baada ya mechi hizo sita, mechi itakayofuatia ya ligi kwa Liverpool watakwenda uwanjani Etihad na kama Klopp na chama lake atakuwa ameshinda hizo mechi zote, basi Pep Guardiola na mastaa wake hawatakuwa na jambo jingine la kufanya kwenye mechi hiyo zaidi ya kujipanga tu mistari miwili kuwapigia makofi mabingwa wakiwa wanaingia uwanjani.
 
Kampeni hiyo ya mechi za kibingwa itaanzia Jumamosi, watakapokipiga nan Norwich City, kisha watakipiga na West Ham uwanjani Anfield, Februari 24 baada ya kumalizana na Atletico Madrid kwenye mtoano wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, mechi itakayopigwa Februari 18. Februari 29, Liverpool watatoka kuwafuata Watford kabla ya kurudi nyumbani Machi 7 kumalizana na Bournemouth.
 
Back
Top Bottom