Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Aina za mawe ya figo

Kuna aina nne ya mawe ya figo:

1. Aina ya kwanza ni yale mawe hutokea wakati mkojo una asidi nyingi. Haya ndiyo mawe ambayo hutokea mara nyingi kuliko mengine yote.Asilimia sabini hadi themanini huwa ni ya aina hii. Mawe haya huwa na asili ya calcium oxalate au calcium phosphate.(Calcium stones ).
 
Mawe ambayo hutokea mkojo unapokuwa na asidi nyingi ya aina ya yuriki,inayotokana na kula nyama nyingi,kuishiwa na maji au kutibiwa saratani.Aina hii ya mawe huwa haiwezi kuonekana kwa picha za ekserei.Asilimia kama tano hadi kumi ya mawe huwa ya aina hii (Uric Acid Stones ).
 
Kila mtu anaweza kupata mawe kwenye figo.Hata hivyo, kuna mambo kadha yanayochangia hali hii:

Kutokunywa maji ya kutosha.

Historia ya familia kupata mawe ya figo.

Kula vyakula vyenye nyama, sodiam, oxalate na maziwa mengi na kukosa mboga na matunda.

Asilimia 75% ya mawe kwenye figo na asili mia 95% ya mawe kwenye kibofu cha mkojo huwapata wanaume kati ya umri wa miaka ishirini na sabini na sana sana walio na uzito mkubwa.
 
Watu wanaoishi sehemu kavu/kame zenye joto jingi.

Watu ambao hawajiwezi na muda mwingi wamelala (bed ridden/ immobile).

Maambukizi ya njia ya mkojo ya mara kwa mara,au kuzibika kwa njia ya mkojo.

Magonjwa kama ya tezi dundundio(thyroid), jongo, na mengineyo yanayotokana na kasoro katika uvunjajivunjaji wa kemikali mwilini.

Matumizi ya dawa fulani fulani kama vile za kukojoa au za kuzuia asidi(diuretics na antiacids).
 
Dalili za mawe katika mfumo wa mkojo ni nini?

Dalili zinazojitokeza hutofautiana kulingana na ukubwa wa jiwe,umbo na mahali lilipo.Dalili zenyewe huwa ni kama zifuatavyo:

Maumivu ya tumbo.
Kukosa dalili zozote na hali hii Hujulikana mtu anapopimwa kwa sababu nyingine. Haya mawe huitwa ‘mawe kimya’.
Kukojoa na kuhisi kutaka kukojoa kila mara.

Kichefuchefu na kutapika.

Kukojoa damu(haematuria).
Uchungu au kuwashwa unapokojoa.
Kama jiwe likikwama kwenye njia ya mkojo,mkojo hukatika ghafla wakati wa kukojoa.

Kukojoa jiwe.
Wakati mwingine jiwe husababisha matatizo kama maambukizi yanayo jirudia rudia kwenye njia ya mkojo, kufunga njia ya mkojo na hivyo kuleta madhara ya muda au ya kudumu kwenye figo ambayo yakakosa kurekebishika.
 
Gari ya mbunge wa Bubu Zanzibar mh Mohamed Raza ikiwa imepata ajali, imefunikwa na tawi la mwembe.
FB_IMG_1581509965835.jpeg
 
Maumivu ya tumbo yanayosababishwa na jiwe katika mfumo wa mkojo

Ukali ya maumivu huwa tofauti kati ya mtu mmoja na mwingine ikitegemea aina,ukubwa na mahali jiwe lilipo.Kumbuka maumivu hayalingani na ukubwa wa jiwe . Jiwe dogo lisilo laini husababisha maumivu makali kuliko jiwe kubwa ambalo ni laini.
 
Je,mawe ya figo yanaweza kuharibu figo?

Ndio. Mawe kwenye figo au kwenye njia ya mkojo yanaweza kuzuia mkojo kutoka na basi kusababisha figo kupanuka (dilatation) .Figo ikipanuka kwa muda mrefu huishia kuharibika. Utambuzi wa mawe kwenye mfumo wa mkojo Uchunguzi hufanywe ili kutambua uwepo wa mawe, matatizo yanayoambatana na hali hii na pia kujua chanzo cha kuwepo kwa mawe haya.
 
Back
Top Bottom