Kila mtu anaweza kupata mawe kwenye figo.Hata hivyo, kuna mambo kadha yanayochangia hali hii:
Kutokunywa maji ya kutosha.
Historia ya familia kupata mawe ya figo.
Kula vyakula vyenye nyama, sodiam, oxalate na maziwa mengi na kukosa mboga na matunda.
Asilimia 75% ya mawe kwenye figo na asili mia 95% ya mawe kwenye kibofu cha mkojo huwapata wanaume kati ya umri wa miaka ishirini na sabini na sana sana walio na uzito mkubwa.