Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

464930984_209497.jpeg
 
KWANINI PESA HAKUNA MTAANI!

Mradi wa Reli ya Kati ya SGR USD Bilioni 7.5 - Fedha UWEKEZAJI WA UBIA ( PPP ) kutoka Benki ya Exim ya China ulikataliwa na Rais MagufuliJP akiamini kuwa ni dili la mtangulizi wake. Akasema tutajenga wenyewe kwa kutumia Kodi. Tukamwambia haiwezekani (Assets-Liabilities Match ).
 
Akaanza kujenga. Hela zikatoka kwenye mzunguko. Hali ya maisha ya wananchi ikawa mbaya, ukuaji wa mzunguko wa Fedha ( M3- money supply ukawa NEGATIVE). Serikali ikaanza kushindwa kulipa invoices za Mkandarasi, wakandarasi wadogo wakakimbia. Ujenzi ukasimama! Moro-Dom ikakwama
 
SGR kipande cha Dar-Moro kilikuwa kiishe Novemba, sasa kipo 70%. Kuisha mwaka kesho. Sasa mkopo wa Biashara wa Fedha za kigeni umechukuliwa. Riba 9%. Serikali ipo kwenye panic. Gharama za Ujenzi zinaongezeka ( costs over run ). Mbia mmoja wa Ujenzi ( Mreno) kabwaga manyanga

Uchumi unaanguka kwa sababu ya viongozi kukosa MAARIFA. Tunapaswa kuikoa nchi yetu sasa sio kesho. #MwagaPombe2020
 
Inasemekana shairi hili lilitungwa na mwalimu mmoja wa Kinyaki (jina nimemsahau). Baada ya shairi kuwa maarufu sana kulikuwa na vuguvugu la kutaka kumtambua mtunzi na kumpa credit. Sijui juhudi hizo zilifikia wapi. Alifariki mwaka juzi/jana...

Kama Mnataka Mali

1. Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafe maishani.

2. Akatamka mgonjwa, ninaumwa kwelikweli,
Hata kama nikichanjwa, haitoki homa kali,
Roho naona yachinwa, kifo kimenikabili,
Semeni niseme nini, kiwafae maishani.

3. Yakawatoka kinywani, maneno yenye akili,
Baba yetu wa thamani, sisi tunataka mali,
Urithi tunatamani, mali yetu ya halali,
Sema iko wapi mali, itufae maishani?

4. Baba aliye kufani, akajibu lile swali,
Ninakufa maskini, baba yenu sina hali,
Neno moja lishikeni, kama mnataka mali,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.

5. Wakazidi kumchimba, baba mwenye homa kali,
Baba yetu watufumba, hatujui fumbo hili,
Akili zetu nyembamba, hazijajua methali,
Kama tunataka mali, tutapataje shambani?

6. Kwanza shirikianeni, nawapa hiyo kauli,
Fanyeni kazi shambani, mwisho mtapata mali,
Haya sasa buriani, kifo kimeniwasili,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.

7. Alipokwisha kutaja, fumbo hili la akili,
Mauti nayo yakaja, roho ikaacha mwili,
Na watoto kwa umoja, wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.

8. Fumbo wakatafakari, watoto wale wawili,
Wakakata na shauri, baada ya siku mbili,
Wote wakawa tayari, pori nene kukabili,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.

9. Wakazipanda shambani, mbegu nyingi mbalimbali,
Tangu zile za mibuni, hadi zitupazo wali,
Na mvua ikaja chini, wakaona na dalili,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.

10. Shamba wakapalilia, bila kupata ajali,
Mavuno yakawajia, wakafaidi ugali,
Wote wakashangilia, wakakumbuka kauli,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.

11. Wakanunua na ng'ombe, majike kwa mafahali,
Wakapata na vikombe, mashine na baiskeli,
Hawakuitaka pombe, sababu pombe si mali,
Kama mnataka mali, mtaipata shambani.

12. Wakaongeza mazao, na nyumba za matofali,
Pale penye shamba lao, wakaihubiri mali,
Wakakiweka kibao, wakaandika kauli...

" Kama mnataka Mali mtaipata Shambani".
Shukrani mpendwa 🙏🙏
 
Back
Top Bottom