Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Zifuatazo ni Baadhi ya Sehemu Ambazo Unatumia Kupoteza Rasilimali Muda
1. Kuangalia Tv
Watu wengi wamekuwa wakipoteza muda sana kuangalia tv, mtu anapoteza masaa matatu mpaka matano kuangalia tv akifuatilia tamthilia kwenye tv. Kuangalia vipindi ambavyo havina tija kwako vipindi ambavyo havina matokeo chanya kwako, kiongozi wa kanisa Katoliki duniani papa francis, ana miaka 25 sasa hajawahi kuangalia tv yaani luninga mara ya mwisho kuangalia tv ilikuwa ni tarehe 15 mwezi saba mwaka 1990. Je tunajifunza nini kutoka kwa kiongozi huyu? Kama yeye ni kiongozi mkubwa wa kanisa hilo duniani mbona hajapungukiwa wala hajapitwa kwa nini wewe usiweze?
 
Kufuatilia Udaku
Unapoteza muda kumfuatilia msanii Fulani leo amefanya nini badala ya kutumia muda huo kuboresha maisha yako. Watu wengi ni wazuri kufuatilia magazeti ya udaku, habari za udaku, mitandao au blog za udaku kuliko kufuatilia blog nzuri zinazotoa elimu ya jinsi kuboresha maisha yako moja wapo ni hii unayosoma makala hii nzuri. Utumie muda wako kufuatilia vitu vya maana ambayo vinabadili fikra yako acha kuwa mtumwa wa kila siku wa kufuatilia habari za udaku.
 
Kufuatilia Mitandao ya Kijamii kwa Faida Hasi
Kuwa katika mitandao ya kijamii kama vile facebook, twitter, na kadhalika siyo mbaya, je uko katika mitandao hiyo ya kijamii kwa malengo gani? Unatumiaje muda wako katika mitandao hiyo ya kijamii kila dakika uko online kwenye mtandao zaidi ya mmoja unapata muda wapi wa kufanya kazi yako kwa ufanisi? Tenga muda wako vizuri kataa kabisa kuwa mtumwa wa kisaikolojia ukikaa kidogo bila kuingia unahisi unapitwa na habari wenzako wanaingiza siku wewe unafuatilia habari.
 
Kukaa Vijiweni
Wimbi la watu kukaa vijiweni na kupoteza muda linaongezeka kila siku ukipita kona hii utakuta watu wamekaa makundi vijiweni wakijadili serikali pengine sijui chama Fulani wamefanya hivi ni mambo mengi yanayojadiliwa kwenye magenge ya watu. Watu hawana kazi za kufanya wanapoteza muda bure na wala hajutii kwa muda anaoupoteza. Tumia muda huo kujifunza namna gani unaweza kubadili maisha yako. Acha kauli hizi za kusema ngoja niende kwa Fulani au kijiweni nikapoteze muda kidogo.
 
Kubishana
Hii ni sehemu moja wapo ambayo watu pia wanapoteza rasilmali yao nzuri ya muda katika kubishana. Watu wanabishania vyama vya siasa, timu za mipira kuna wengine wanabishana katika mpira mpaka wanapigana hii ni kwa sababu kila mmoja anataka asikilizwe kile anachosema yeye katika timu yake ndio sahihi. Unapoteza muda kushabikia vitu wakati huna hata hisa moja katika vitu hivyo unavyobishania ambavyo havikusaidii kuboresha maisha yako kabisa zaidi ya kukusababishia hasara ya kuendelea kuwa mtumwa wao.
 
Umbea na Majungu
Unapoteza muda kuongea maneno ya uchonganishi juu ya mtu Fulani unapiga umbea na majungu. Unaongea maneno ambayo yanaleta majeraha katika maisha ya watu, unapandikiza chuki kwa watu kwa kupiga majungu unapoteza muda wako bure kupiga umbea na majungu bila malipo yoyote ni hatari sana tumia muda wako kujenga na kuongea thamani yako katika jamii ya yako na acha kuwa mtu wa umbea na majungu kila siku.
 
Kuhudhuria Vikao au Mikutano Ambayo Haikupi Faida
Kuna vikao vingi sana katika jamii zetu, mikutano mingi ya kila siku ambayo haina matokeo chanya kwetu bali ni kupoteza wakati wako. Leo nakuomba sema HAPANA kwa vikao au mikutano ambayo haikupi faida yoyote ambavyo vinakula muda wako bure ambao muda huo ungeweza kutumia vizuri kuboresha maisha yako au hata kuongeza thamani katika jamii yako.
 
Hivyo basi, acha kutumia muda wako kudhurura ovyo yaani kutembea bila sababu ya msingi, tumia muda wako vema, muda ni mali katika karne hii usikubali mtu akupotezee muda kwa kitu ambacho hakina manufaa kwako fanya kile ambacho unatamani kufanya kwa muda huu katika Nyanja zote usisubiri ruhusa ukiendelea kusubiri ruhusa ndio unazidi kupoteza muda na umri pia unakwenda omba samahani kuokoa muda, Muda siyo rafiki na maisha ni mafupi .
 
Katika dunia ya sasa ni kawaida sana kukutana na mtu akimthamini na kumjali mtu kwa kuwa ipo faida anaipata au ananufaika kwa njia moja au nyingine. Mfano huenda ni katika eneo lako la kazi, pengine bosi wako kwa kuwa tu wewe ni mfanyakazi mzuri basi ataonekana kukubali na kukuheshimu sana tu kumbe anafanya hayo kwa kuwa tu ipo faida anaipata kwa uwepo wake mahali pale pa kazi, pengine usipokuwepo naye nafasi yake itakuwa hatarini maana ni mapengo mengi unayaziba na kumfanya aonekane kuwa bora sana mahali pake pa kazi, unampa thamani mahali pale, hivyo naye anaonekana kukuthamini tu kwa kuwa ana anachopata kwako. Ile thamani uliyo nayo inamlazimisha kukujali na hata kukutumia zaidi.
 
Au kwa wanafunzi unapokuwa shuleni unakuta kuna mwenzio ana uwezo zaidi kwenye somo fulani hivyo unakuta mtu yule anategemewa na wengi na anaweza kuonekana kupendwa na wengi kwa kuwa anawasaidia wengi kuweza kufanya vizuri kwenye masomo anayowasaidia kuwafundisha ili waweze kuelewa zaidi, ukiangalia kwa kawaida unaweza ona kama yule mtu anapendwa na wengi, lakini ukiangalia zaidi utagundua pale hapendwi mtu bali kipo kitu cha thamani ambacho kinapendwa kwa mtu yule, kipo kitu watu wanakifuata kwa mtu yule ambacho pengine kwa wakati ule hakuna mahali pengine tena wataweza kupata kitu hicho, hivyo naweza sema wanakuwa hawana namna mbadala ya kupata huduma ile, wanalizimika kumkubali mtu yule hata kama hawampendi, wanalazimika kumsikiliza na wanakubali kufundishwa naye maana hakuna mwingine anaweza kufanya lile.
 
Pengine unaweza kukutana na mtu ukamshangaa na usimwelewe kwa kuwa anaambatana na mtu fulani, pengine wewe ukiangalia kwa macho yako ya kawaida unakuwa huioni thamani ya huyo mtu, huoni cha maana alichonacho cha kumfanya mtu mwingine asitake kuwa mbali naye, unajitahidi sana kukiona hicho lakini huoni, lakini wewe ukiwa katika hali hiyo kuna mwingine ameona thamani kwa huyo mtu, na anajua namna ya kuipata, hivyo anahakikisha anamtumia huyo mtu kuweza kupata kile mtu anacho, anamtumia yule mtu kuweza kufika pale anaelekea, usiishie kushangaa ni kwa nini mtu fulani anamkubali sana yule, usiwe mwepesi kumpuuza au kuona amepotoka wakati huelewi hasa ni kwa nini anafanya vile.
 
Kama ukiwa mwelewa na mjanja mwenye nia ya kujifunza na kueleweshwa utatumia hekima na busara ili kuweza kuona kile mwenzio anaona kwa huyo mtu, utauliza na ukielekezwa uwe tayari kuheshimu hata mawazo ya wengine, uweze kuona thamani hata kwa wengine, hata kama wewe unadhani unajua kila kitu lakini tambua wapo wengine pia wanaoweza kuwa na uelewa kuliko wewe.
Wakati mwingine unaweza kukutana na mtu na ukamshangaa kwa nini anaambatana na mtu fulani maana wewe kwa viwango vyako na vipimo vyako unaona yule mtu si sahihi au hana sifa za kuweza kuwa na mtu yule na pengine unaweza kujaribu hata kumshawishi asiwe na mtu yule, pengine hata kwa kumweleza ni jinsi gani unaona hafai kwa kuelezea yale mabaya yake au madhaifu yake lakini cha ajabu unashangaa pamoja na hayo bado mtu yule anaendelea na msimamo wake wa kuambatana na mtu yule.
 
Tambua yule ni mtu mwenye uelewa wa kutosha naamini ni yeye anaelewa ni kwa nini anaambatana na mtu yule, anajua ni kwa nini anashirikiana na mtu yule kwenye shughuli zake, yeye ndiye anajua ameona nini kwa mtu yule, pengine wewe huoni thamani kwa mtu yule, lakini yeye ameiona hiyo na hiyo ina nguvu kuliko sauti yako ya kumwaminisha kinyume, sauti yako anaona kama kelele tu, unatakiwa ujiulize unavyomwambia hayo wewe unaonekanaje kwa mtu huyo? Kwanini aamini unayosema? Una nini cha kukufanya aamini unachosema? Je una sababu za msingi za kuona yule mwingine hafai? Huyo ambaye hafai unamwelewaje? Unamfahamu sawasawa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…