Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kuoza kwa kuta
Moja ya masahibu yanayoyakumba majengo ni kuoza kwa kuta za tofali au chuma. Hali hii hutokana na unyevunyevu na kemikali mbalimbali kupitia maji kukaa kwa muda mrefu kwenye kuta hali inayoathiri ubora wakuta hizo. Pia hali hiyo husababishwa na kumea kwa mimea au kupanda maua kwenye viambaza vya kuta ambapo baadhi ya mimea hiyo kusababisha ukungu wa kijani kwenye kuta ambao huzalisha fangasi mbalimbali wanaokula kuta. Pia kitendo cha kumwagilia maua kwenye kuta huozesha kuta haraka. Kinga kuta zote zithiathiriwe na hali ya hewa na maji pale inapolazimu na Usiruhusu mimea kumea kwenye viambaza vya kuta.
 
Kuoza kwa paa
Unapaswa kutambua kuwa kila kilichoumbwa kina mwisho, ndivyo ilivyo hata kwenye majengo, kila aina ya malighafi iliyotumika hufika mwisho wake kwa wakati tofauti kulingana na ubora na namna yalivyotumika katika ujenzi. Kuoza kwa paa hutegemea ubora na aina ya malighafi zilizotumika bila kusahau na kimo cha mwinuko wa paa hilo. Paa huathiriwa na hali ya mazingira ya eneo husika, mfano paa zilizopo ukanda wa pwani huthiriwa na chumvichumvi zinazobebwa na mikondo ya upepo uvumao kutoka baharini hali inayosababisha paa kuoza haraka, pia hali ya mwinuko ukiwa mdogo husadia paa kuhifadhi takataka mbalimbali ikiwemo majani ya mimea, hali hii ya uchafu kukaa muda mrefu huozesha paa haraka. Unapaswa kuweka paa lenye ubora kulingana na mazingira halisi. Inasikitisha kuona hadi leo hii bado kuna nyumba za serikali zimeezekwa vigae vya asbestos ambavyo ni hatari na vimepigwa marufuku kwa matumizi ya binadamu.
 
Kusinyaa na kutanuka kwa milango na madirisha
Kuna shida sana hapa, watu wengi hujikuta wakiwalalamikia sana mafundi kuwa hawafai na wamewatia hasara. Kuna aina nyingi za malighafi zinazotumika kutengenezea milango na madirisha, kila aina ya malighafi hizo zina faida na hasara zake. Karibu aina zote za malighafi zina tabia ya kusinyaa na kutanuka kutokana na hali ya hewa (jotiridi) ya mazingira nyumba zilipo. Tumia mbao ngumu (treated hardwood) ili kuondokana na tatizo hili, usitumie mbao mbichi zitakusumbua sana siku zijazo.
 
Kwa wale wanaotumia madirisha na milango ya vioo na aluminiam ni lazima wayapachike na kufitisha kwenye mbao na siyo moja kwa moja kwenye kuta ili kuruhusu hali ya kusinyaa na kutanuka, usipo fanya hivyo aluminiam hupinda na kuleta shida ya kufunga na kufungua. Pia kama unatumia madirisha haya ya vioo (sliding windows) ni lazima yawe makubwa ili kuruhusu hewa kuingia na kutoka kwa haraka kwa kuwa madirisha haya hufunguka nusu tu. Kumbuka kuweka vitasa sahihi kulingana na matumizi, Zingatia sana haya kwa kuwa kila unachoweka kwenye nyumba ni fedha hivyo usiache watu wafanye hovyohovyo tu, ni kero na hasara, wewe na wateja wako hamtafurahia mazingira ya nyumba hiyo.
 
ni mwisho wa wiki sasa, kumbuka kufanya tathmini ya mambo uliyoyafanya wiki nzima, pitia malengo yako ya wiki hii kama yote yametimia na ongeza juhudi kukamilisha mipango yako ili uweze kufikia malengo ya mwaka uliyojiwekea. Napenda nikukumbushe kuwa kila siku unayoianza ni siku ya kipekee, haitaweza kurudia tena maishani mwako, ni zawadi nzuri sana ambayo Mungu amekupa. Tumia kila siku vizuri, uwe na furaha na uguse maisha wengine pia.
Maisha ni safari. Sio mara ya kwanza kuusikia usemi huu. Naomba leo nikupe mtazamo mwingine kuhusu usemi huu.
 
Ankoo mbona unataka kuifanya iwe kesi kubwa wakati tupo tunaongea tu. In fact hili ndilo jibu alitakiwa kutoa muuliza swali. Ila msianze kusema nawapangia majibu [emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Mwenyewe nimedandia treni kwa nyuma hata sijasoma kibao...
Maisha ya hapa ni ya kawaida sana tuchukuliane kirahisi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji1][emoji1][emoji1][emoji1][emoji1]
Mwenyewe nimedandia treni kwa nyuma hata sijasoma kibao...
Maisha ya hapa ni ya kawaida sana tuchukuliane kirahisi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Maisha ni rahisi sana hapa, kila mtu anapost apendacho hata mtu akikuuliza si kwa ubaya kiasi tufike hadi kuambiwa tubonyeze ignoa listi[emoji16][emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…