Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Desemba 31
Siku moja ya baada ya kumpiga kijembe Solskjaer, Raiola safari hii aishukia Man United akidai Pogba anatakiwa kucheza timu inayoshinda mataji na inashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuushangaa uongozi wa klabu hiyo kwa kukaa tu bila kuchukua hatua wakati timu inazidi kupotea. Siku hiyo hiyo anaenda mbali zaidi na kusema hatampeleka mchezaji yeyote Old Trafford kwa sababu kwa sasa timu hiyo inaweza kuua kipaji hata cha Diego Maradona, Pele na Paolo Maldini.
 
Januari 1
Rio Ferdinand aingia vitani na kumponda Raiola, huku akisema: β€œNingekuwa mtu ambaye namshauri Paul (Pogba), ningemwambia nenda kazungumze ishu zako mwenyewe usimruhusu wakala wako aongee, mfunge mdomo.”
 
Januari 2
Raiola aishukia tena United, akisema: β€œSikumlazimisha kwa silaha mtu yeyote pale Manchester United kumsajili Paul Pogba, Alex Ferguson alinipinga mimi na Paul, hilo linaruhusiwa, lakini alikuwa wapi walipomrudisha.”
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]nmeona ankoo na bro kama wanafaidi sana na story zao,nikaona isiwe kesi acha nijoin nao[emoji23][emoji23]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]na ukaingia pupa mpaka wamekushtukia. Maana story zao wanatunga hata waliyohadithiwa enzi za mababu zao na sie tunakubali tu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Februari 17
Dakika 17 kabla ya mechi ya Ligi Kuu England kati ya Chelsea dhidi ya Man United, Raiola anajibu mapigo kwa Solskjaer, kupitia ukurasa wake wa Twitter, akisisitiza kwamba Pogba si mfungwa na hamilikiwi na yeye wala Solskjaer na ana haki ya kuamua nini anataka kufanya, huku akimdhihaki Solskjaer kwa kusema kocha huyo amechanganywa na mambo yanavyoenda ndani ya klabu hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…