Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

10. Andriy Shevchenko - Chelsea, Euro 44 milioni
Hakuna anayebisha kwamba Shevchenko alikuwa mmoja wa kati ya washambuliaji bora kabisa kuwahi kutokea kwenye soka la Ulaya. Alikuwa moto huko AC Milan, lakini alipohamia tu Chelsea kwa pesa ndefu wakati huo, mambo yalikwenda kuharibika.
 
9. Christian Benteke - Liverpool, Euro 46.5 milioni
Mwaka 2015 straika Benteke alikuwa kwenye orodha ya timu vigogo zilizokuwa zikitaka mastaa hatari wa kufunga. Alifunga mabao 43 kwenye misimu yake mitatu aliyokuwa na Aston Villa kwenye Ligi Kuu England. Liverpool ikaona anawafaa, wakamsajili, kwa pesa ndefu, lakini baada ya usajili huo tu ikawa majanga. Msimu mmoja aliokuwa Anfield aliishia kufunga mabao tisa tu na alipokuja Kocha Jurgen Klopp ikawa hata kucheza hachezi, akapigwa bei Crystal Palace.
 
8. Fernando Torres - Chelsea, Euro 58.5 milioni
Bila shaka, ni moja kati ya usajili wa pesa nyingi uliochemsha zaidi. Lakini, kwa bahati nzuri kwake alishinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Europa League akiwa na kikosi cha Chelsea. Straika Fernando Torres hakufurahia maisha binafsi kwenye kikosi cha Chelsea baada ya kujiunga kwa pesa ndefu, ambapo alikomea kufunga mabao 20 tu kwenye Ligi Kuu England na 10 kwenye Ligi Kuu England baada ya miaka mitatu na nusu. Akatolewa kwa mkopo kwenda AC Milan kabla ya kuuzwa kabisa.
 
7. Fred - Man United, Euro 59 milioni
Walau kwa sasa kuna kitu tofauti amekuwa akikifanya Fred ndani ya uwanja huko katika kikosi cha Manchester United.
Jose Mourinho alihitaji kiungo wa boksi kwa boksi kwenye kikosi chao akaona Mbrazili, Fred anamfaa, lakini baada ya kutua tu, kila kitu kilikuwa tofauti na kiungo huyo hakuwa na makali uwanjani.
Mourinho aliondoka na kutua Ole Gunnar Solskjaer, ambaye pia siku za mwanzo alimpiga sana benchi kiungo kabla ya kupata majeruhi kwenye kikosi waliomfanya Fred aanze kucheza.
 
7. Fred - Man United, Euro 59 milioni
Walau kwa sasa kuna kitu tofauti amekuwa akikifanya Fred ndani ya uwanja huko katika kikosi cha Manchester United.
Jose Mourinho alihitaji kiungo wa boksi kwa boksi kwenye kikosi chao akaona Mbrazili, Fred anamfaa, lakini baada ya kutua tu, kila kitu kilikuwa tofauti na kiungo huyo hakuwa na makali uwanjani.
Mourinho aliondoka na kutua Ole Gunnar Solskjaer, ambaye pia siku za mwanzo alimpiga sana benchi kiungo kabla ya kupata majeruhi kwenye kikosi waliomfanya Fred aanze kucheza.
 
6. Alvaro Morata - Chelsea, Euro 66 milioni
Chelsea imekuwa na utamaduni wa washambuliaji wake wa kati kushindwa kufanya vyema. Alvaro Morata ameshindwa kujiengua kwenye orodha hiyo. Bilionea Roman Abramovic alivunja benki kupata saini yake na kuamini kwamba, atakwenda kuwa mshambuliaji matata kwenye kikosi chake, lakini mambo yamekuwa tofauti na yalivyotarajiwa.
Morata hakuwa kabisa tishio kwenye kufunga mabao na alijikuta akiondoka kwenye kikosi nafasi yake akichukua Olivier Giroud. Alitolewa kwa mkopo Atletico Madrid kisha akauzwa kabisa.
 
5. Kaka - Real Madrid, Euro 67 milioni
Kaka alikuwa mmoja kati ya wachezaji bora kabisa duniani miaka 10 iliyopita. Ubora wake huko AC Milan uliwasukuma Real Madrid kutoa pesa ndefu kuinasa saini yake katika mwaka ambao ilimsajili pia Cristiano Ronaldo.
Baada ya kufika tu Hispania, kwa bahati mbaya, Kaka hakuwa tena kwenye ubora wake. Miaka minne kwenye kikosi hicho cha Bernabeu, akaandamwa tu na majeraha na matokea yake akarudi kwenye klabu yake ya zamani ya AC Milan.
Na tangu hapo, Kaka alishindwa kurudi kwenye ubora wake.
 
4. James Rodriguez - Real Madrid, Euro 75 milioni
James Rodriguez, alikuwa kinara wa mabao kwenye Kombe la Dunia 2014. Lilikuwa ni jambo lisilozuilika kumwona akinaswa na Real Madrid kwa pesa ndefu. Lakini, pia haikuzuilika kumwona akiondoka kwa mkopo kwenye timu hiyo misimu mitatu baadaye.
Rodriguez alikuwa na wakati mzuri kwenye kikosi cha Madrid chini ya Kocha Carlo Ancelotti, lakini baada ya kuja kwa Zinedine Zidane tu kila kitu kilikuwa tofauti.
Akaanza kikosa nafasi ya kucheza na hakuwa na kitu cha ziada kufanya uwanjani kudhihirisha ubora wake.
 
3. Angel Di Maria - Man United, Euro 75 milioni
Manchester United ilikubali kutoa pesa ndefu kuinasa huduma ya winga wa Kiargentina, Angel Di Maria baada ya kukoshwa na kile alichokuwa akikifanya huko Real Madrid. Di Maria alikuwa balaa uwanjani, ambapo aliisaidia Real Madrid kubeba ubingwa wa Ulaya na hapo Man United ikanasa saini yake na kumkabidhi jezi yenye Namba 7, ambayo inahadhi kubwa huko Old Trafford. Lakini, kwenye kikosi cha Man United, Di Maria hakuwa na maajabu na akapigwa bei baada ya msimu mmoja tu kwenda Paris Saint Germain.
 
2. Ousmane Dembele - Barcelona, Euro 115 milioni
Ilikuwa rahisi kuwashangaa Barcelona uamuzi wao wa kutoa pesa ndefu kunasa saini ya Ousmane Dembele. Wengi wanasema Barca walipaniki kwenye kuziba pengo la Neymar, aliyetimkia zake Paris Saint-Germain.
Ukweli, Dembele baada ya kutua Nou Camp hakuna kikubwa alichokifanya na muda mwingi amekuwa nje ya uwanja kutokana na kuwa majeruhi ikiwamo hivi sasa, ambapo hatacheza tena hadi mwisho wa msimu.
Kwenye dirisha lililopita, jina la Dembele lilihusishwa sana kwenye orodha wanaoweza kuuzwa.
 
1.Phillipe Coutinho - Barcelona, Euro 145 milioni
Barcelona inaonekana kama vile ni vinara wa tabia ya kutumia pesa hovyo. Miaka michache iliyopita walinasa huduma ya staa wa Kibrazili, Coutinho kutoka Liverpool kwa ada ya Euro 145 milioni. Haikuwa pesa ya kitoto unaambiwa kwani, akaunti ilivunjwa.
Pesa ndefu ilitoka, Barca ikiwa kwenye mchakato wake wa kuziba pengo la Neymar, lakini mambo yamekuwa tofauti.
Coutinho hakuwa na jipya la kufanya kwenye kikosi hicho cha Nou Camp na kujikuta akitolewa kwa mkopo kwenda Bayern Munich, ambako pia amechemsha na sasa anahusishwa na mpango wa kurudi England kukipiga tena huko Liverpool.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…