Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Straika wa Barcelona, Suarez amehusika kwenye mabao 82 katika mechi 83 akifunga mabao 57 na kuasisti 25, wakati kinda wa PSG, Mbappe amehusika kwenye mabao 80, akifunga mara 61, asisti 19 katika mechi 75 huku Aguero aliyecheza mechi 79 ndani ya muda huo amehusika kwenye mabao 75 sawa na Aubameyang wa Arsenal. Aguero amefunga mabao 58 na kuasisti 17, wakati Aubameyang kwenye mechi 90 alizocheza, amefunga mabao 62 na kuasisti 13.
 
Straika wa Bayern Munich, Lewandowski anafuatia akiwa amehusika kwenye mabao 88 katika mechi 86 alizocheza ambapo amefunga mabao 76 na kuasisti 12, wakati staa wa Juventus, Ronaldo amehusika na mabao 83 ndani ya muda huo, ambapo amecheza mechi 79, akifunga mabao 68 na kuasisti 15.
 
Staa wa Kibrazili, Neymar anakamilisha orodha ya washambuliaji 10 moto waliohusika kwenye mabao mengi, ambapo mkali huyo wa PSG amefunga mabao 47 na kuasisti mara 26 katika mechi 52 alizocheza na hivyo kuhusika na mabao 73 ndani ya muda huo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…