Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kwenye mpango huo, Los Blancos wameripotiwa kuandaa mkwanja wa Pauni 127 milioni wakiamini kabisa utatosha kuinasa saini ya Mo Salah, lakini kama watahitaji huduma ya Mbappe, basi watalazimika kutoa pesa nyingi zaidi.
 
Hata hivyo, kwenye mpango huo hatima ya wachezaji wote hao wawili katika mpango wa kutua Bernabeu utatokana na bei atakayouzwa Gareth Bale, ambaye amekuwa akiteseka kupata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha Kocha Zinedine Zidane.
 
Mo Salah ndiye anayepewa nafasi kubwa kutokana na kwamba atapatikana kwa bei ndogo, huku huduma yake ikiwamo moto, ambapo amefunga mabao 90 katika mechi 140 alizoitumikia Liverpool tangu alipowasili kutoka Roma, ikiwamo mabao 19 katika mechi 36 za michuano yote aliyocheza kwenye msimu huu wa 2019-20.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…