Staa mwingine ni Alexis Sanchez, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo huko Inter Milan. Man United inataka kuachana na mchezaji huyo ili kuokoa Pauni 505,000 inazomlipa kwa wiki. Wakati sasa akiwa Inter, Man United inamlipa mshahara wa Pauni 300,000 kwa wiki, ikiwa ni pesa nyingi kwa mchezaji asiyekuwa na faida. Hata huko Inter ni majanga, ambapo amefunga mara moja tu katika mechi 13 alizocheza na ameshaonyeshwa kadi nyekundu.