Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Klabu hiyo ya Beckham inaanza kucheza msimu wake wa kwanza kwenye Ligi Kuu Marekani mwaka huu. Akiwahi kuwa mchezaji mkubwa kwenye soka, ambapo alitamba na klabu za Manchester United na Real Madrid kwa kuzitaja kwa uchache, mpango wa Beckham ni kuvuta mastaa wenye majina makubwa kwenye klabu yake hiyo ya Miami.
 
Kila timu duniani ingehitaji kuwa na huduma ya Messi na Ronaldo kwenye vikosi vyao. Lakini, siku zote tumekuwa tukijizungumzia sisi kuwa timu tofauti na nyingine, kitu ambacho naamini hata waamini wa klabu nyingine nao watakuwa wanasema kitu kama hicho.
 
Hivyo basi tunajaribu jambo hilo na kama tutakuwa na nafasi ya kuleta mastaa wakubwa kwenye timu itakuwa bahati yatu na tunataka kufanikiwa hivyo tunahitaji kuleta wachezaji bora."
Beckham aliwahi kuzichezea pia AC Milan, Paris Saint-Germain na LA Galaxy katika maisha yake ya soka.
 
Solskjaer amefanya usajili wa pesa nyingi kwenye kikosi chake ikiwamo kutumia Pauni 85 milioni kumnasa beki wa kati, Harry Maguire, Pauni 50 milioni kumnasa beki wa kulia Aaron Wan-Bissaka na Pauni 55 milioni kwenye kunasa huduma ya kiungo mshambuliaji, Bruno Fernandes.
 
Orodha ya wachezaji waliopo njiani kutua kwenye kikosi hicho inawahusu Jadon Sancho, Jack Grealish, Dominic Calvert-Lewin na James Maddison kwa kuwataja kwa uchache, lakini kuna kundi la mastaa ambao wataonyeshwa mlango wa kutokea baada ya kuonekana hawana kitu cha ajabu wanachoweza kukifanya kwenye timu.
 
Mastaa hao watano wanaodaiwa watafunguliwa mlango wa kutokea atakuwapo pia Paul Pogba ambaye kwa muda mrefu tangu kwenye dirisha lililopita la uhamisho wa majira ya kiangazi mwaka jana, alitaka kuachana na timu hiyo kwenda kukabiliana na changamoto mpya.
 
Pogba alitua Old Trafford mwaka 2016 kwa ada iliyoweka rekodi ya dunia kwa wakati huo, Pauni 89 milioni, lakini sasa kwenye kumpiga bei, mabosi hao wa Man United wanataka Pauni 150 milioni. Msimu huu, Pogba amecheza mechi saba tu kwenye Ligi Kuu England na hajafunga bao lolote.
 
Staa mwingine ni Alexis Sanchez, ambaye kwa sasa anacheza kwa mkopo huko Inter Milan. Man United inataka kuachana na mchezaji huyo ili kuokoa Pauni 505,000 inazomlipa kwa wiki. Wakati sasa akiwa Inter, Man United inamlipa mshahara wa Pauni 300,000 kwa wiki, ikiwa ni pesa nyingi kwa mchezaji asiyekuwa na faida. Hata huko Inter ni majanga, ambapo amefunga mara moja tu katika mechi 13 alizocheza na ameshaonyeshwa kadi nyekundu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…