Maisha ya lymphoctes yanaanzia ndani ya uboho. Seli nyingine hubaki ndani ya uboho na kugeuka kuwa B lymphocytes (B cells), wakati nyingine huelekea hadi kwenye thymus na kugeuka kuwa T lymphocytes (T cells). Seli za aina hizi mbili hufanya kazi tofauti:
Kinga za mwili zinatakiwa kuwa na uwezo wa kupambanua kati ya seli na tishu za mwili na vitu kutoka nje. Kinga huweza kufanya upambanuzi kwa kuchunguza protini zilizo juu ya seli. Hujifunza kuziacha (kutozidhuru) protini binafsi katika hatua za awali kabisa.
Mara nyingi antigen huwa ni bacteria, fangasi, sumu, chembechembe za vumbi, au kiumbe kingine kutoka nje. Lakini inaweza kuwa ni seli ya mwili yenye dosari au iliyokufa. Seli za aina nyingi kwa pamoja hutambua uwepo wa antigen kama adui.
Kazi Ya B Lymphocytes
Mara baada ya kumwona adui yaani antigen (antigen ni kifupi cha “antibody generators”), B lymphocytes hutoa kingamwili . Kingamwili (antibody) ni protini za kipekee ambazo humzunguka adui.
Kazi Ya B Lymphocytes
Mara baada ya kumwona adui yaani antigen (antigen ni kifupi cha “antibody generators”), B lymphocytes hutoa kingamwili . Kingamwili (antibody) ni protini za kipekee ambazo humzunguka adui.
Kila seli ya B lymphocyte hutoa kingamwili ya aina yake. Kwa mfano seli moja itatoa kingamwili dhidi ya bakteria aletae pneumonia, na nyingine inaweza kutambua kirusi aletae mafua.
Kingamwili (antibodies) ni sehemu ya familia ya kemikali ziitwazo immunoglobulins, ambazo zina kazi nyingi katika ulinzi dhidi ya adui. Kazi ya kingamwili ni kumnasa na kumzungua adui, lakini si kuua. Kuua ni kazi ya seli nyingine, kama phagocytes.
Kazi za T Lymphocytes
Kuna aina tofauti mbili za T lymphocytes:
Helper T cells (Th cells) — Zinafanya kazi ya kuratibu mashambulizi dhidi ya adui. Baadhi huwasiliana na seli nyingine, nyingine huzichochea B cells ili zitoe kingamwili zaidi. Nyingine huziita T cells au seli zinazotafuna seli za adui-phagocytes.
Kila mtu ana kinga za mwili zilizo tofauti na kinga za mtu mwingine, lakini kwa kawaida kinga za mwili huwa imara zaidi mtu anapofikia utu uzima, kwa sababu muda huu, ameshapambana na aina nyingi sana za viini vya magonjwa na kujijengea kinga zaidi.
Hii ndiyo sababu baadhi ya magonjwa, kama tetekuwanga, huja mara moja tu katika maisha ya mtu kwa vile kingamwili za tetekuwanga zilikwisha andaliwa na kuhifadhiwa tayari kutumika pale ugonjwa unaporudi. Hii huitwa kinga ya mwili.
Mtu anapopewa chanjo dhidi ya ugonjwa, antigen au viini vya ugonjwa vilivyodhoofishwa huingizwa ndani ya mwili wake kwa jinsi ambavyo havitaweza kumletea ugonjwa bali atengeneze kingamwili. Kwa vile mwili hutunza kivuli cha kingamwili zilizotengenezwa, utalindwa ikiwa ugonjwa huo utamvamia tena katika maisha yake.
Kwa vile mfumo wa kinga za mwili una vipengele vingi sana, kuna namna nyingi ambavyo unaweza kujikuta haufanyi kazi ipaswavyo. Dosari za kinga za mwili huangukia katika makundi matatu yafuatayo:
Immunodeficiencies. Haya ni matatizo ya ukosefu wa kinga mwilini yatokanayo na sehemu ya mfumo wa kinga mwilini kukosekana au kutofanya kazi vizuri. Watu wengine huzaliwa wakiwa na ukosefu wa kinga – hii huitwa primary immunodeficiency, ingawa dalili zake hujitokeza baadaye sana katika maisha yao. Ukosefu wa kinga mwilini huweza kutokea kwa sababu ya maambukizi ya wadudu au matumizi ya madawa – secondary immunodeficiency.
Immunodeficiencies huweza kuathiri B lymphocytes, T lymphocytes, au phagocytes. Mfano wa primary immunodeficiency inayowaathiri watoto na vijana ni IgA deficiency. IgA ni immunoglobulin ambayo hupatikana katika mate na majimaji mengine ya mwili. IgA deficiency ni hali ambapo mwili hauzalishi kiasi cha kutosha cha kingamwili IgA. Watu wenye IgA deficiency huwa wana matatizo ya mzio au kupata mafua mara kwa mara na maambukizi kwenye mfumo wa upumuaji.