Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

EDEN HAZARD WINGA REAL MADRID
Kwa Neymar winga huyo wa kimataifa wa Brazil na timu ya Real Madrid ndiye mchezaji wa tano kwa ubora kwa sasa duniani, licha ya kwamba hajawahi kucheza timu moja na Hazard, Mbrazil huyo anaamini winga huyu wa zamani wa Chelsea ni fundi sana wa mpira na ndiyo maana kampa nafasi hii.
 
PAUL POGBA KIUNGO MANCHESTER UNITED
Ukisikia jinsi ambavyo Real Madrid na Juventus zinapambana kuisaka saini yake utaelewa kwa nini Pobga yuko katika nafasi ya nne miongoni mwa wachezaji ambao wanajua sana mpira kwa sasa duniani. Bila shaka ile mipasi mirefu, udambwidambwi na nguvu ndivyo vinamfanya Neymar akubali kuwa Mfaransa huyu ni kiungo aliyekamilika.
 
KYLIAN MBAPPE MSHAMBULIAJI PARIS SAINT GERMAIN
Katika umri wa miaka 21, Mbappe tayari anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani kwa sasa akiwa tayari ana medali ya Kombe la Dunia. Unaweza kuelewa kwa nini Mbappe yuko kwenye orodha hii, yuko kikosi kimoja na Neymar, hivyo Mbrazili huyo anamuona kila siku mazoezini na kwenye mechi kwa hiyo anamjua.
 
LUIS SUAREZ MSHAMBULIAJI BARCELONA
Ukitaka kujua kwa nini Suarez yuko kwenye nafasi ya pili angalia jinsi Barcelona inavyohangaika kuziba pengo lake, lakini pia ni mchezaji ambaye aliwahi kuwa sehemu ya kombinesheni hatari na Lionel Messi, Neymar mwenyewe ambayo ilipewa jina la MSN.
 
LIONEL MESSI MSHAMBULIAJI BARCELONA
Si ajabu kuona mshindi mara sita wa Tuzo ya Ballon d’Or akikaa juu kwenye orodha hii, maana siku zote huwezi kutaja wachezaji bora duniani kwa sasa bila kutaja jina la Messi.
Huyu ni mchezaji ambaye ameshinda karibu tuzo zote binafsi na amevunja rekodi za kila aina kwenye soka, bahati nzuri zaidi kwa Neymar amewahi kucheza naye kikosi kimoja, hivyo anaposema ni bora ina maana anajua kile anachokisema.
 
Kinachostaajabisha, licha ya kutumia pesa ndefu kutengeneza vazi hilo, lakini Wilder analalamika kuwa uzito wake ulichangia kupigwa katika pambano hilo lililofanyika Jumapili asubuhi katika Ukumbi wa MGM Grand Arena, Las Vegas, Marekani.
 
Messi ameonyesha ni balaa zaidi, ambapo katika mechi 90 alizocheza ndani ya muda huo amefunga mabao 98 na kuasisti mara 37, hivyo kwa ujumla wake akiwa amehusika kwenye mabao 125. Ndio mechi 90, mabao 125. Hiyo ndio hatari ya Messi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…