Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Mara nyingi harufu itokayo mdomoni, hutokea tumboni na siyo kinywaji peke yake kama unavyoweza kudhani. Hivyo, kama tumbo litakuwa chafu, hata kama utasafisha kinywa vizuri bado harufu mbaya inaweza kuendelea kutoka. Harufu mbaya ya tumboni hutokea pale tumbo linapokuwa chafu kutokana na kutopata choo kwa muda mrefu. Miongoni mwa mambo yanayochangia kukosekana kwa choo kwa muda mrefu ni pamoja na tabia ya kutokunywa maji ya kutosha kwa siku, hivyo hakikisha unakunywa maji, kiasi kisichopungua lita moja na nusu hadi mbili au zaidi, kutegemeana na kazi unazozifanya.
 
Ukiwa na tatizo la kukaukiwa maji mwilini kila mara, mwili hujaribu kutumia njia zake za kiasili kupunguza uzalishaji wa mate ili kuhifadhi maji kwa ajiili ya matumizi mengine, kitendo hicho huchangia kunukisha mdomo kwa sababu ndani ya mate huwa kuna kinga muhimu dhidi ya baktetria wanaonukisha kinywa.
 
MWISHO:
Hakikisha unasukutua sawaswa baada ya kula chakula chochote, hata kama ni juisi isipokuwa unapokunywa maji tu ya kawaida. Bila shaka, ukizingatia haya, tatizo ulilonalo la kunuka mdomo litataoweka na kubaki historia.
 
Mara nyingi huwa tunafikiri wkamba tunaweza kuwadhibiti watu, kudhibiti hali zinazotokea, kudhibiti fedha na mambo mengine mengi. Ila tunapojaribu kudhibiti vizu hivi tunashindwa vibaya sana. Kwa kushindwa huku tunaweza kujiona kama hatufai au hatuwezi kuendesha maisha yetu vizuri.
 
Leo nataka nikuambie kwamba kushindwa kudhibiti vitu hivyo unavyotaka kudhibiti hakumaanishi kwamba maisha yako hayafai. Ila ni kwamba hujajua ni vitu gani unavyoweza kudhibiti na vitu gani huwezi kudhibiti. Kuna kitu kimoja tu ambacho unaweza kukidhibiti kwenye dunia hii na kwenye maisha yako. Kwa mudhibiti kitu hiki kimoja, vitu vingine vyote vinakwenda sawa, hata kama utakuwa hujavidhibiti.
 
Hivyo kama unataka kudhibiti maisha yako, kama unataka kuboresha maisha yako, anza kwa kudhibiti na kuboresha mawazo yako. Kuwa na mawazo ya yale mambo unayotaka, kuwa na mawazo chanya na jione wewe ni wa tofauti na una uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko kwenye maisha yako na ya wanaokuzunguka.
 
TAMKO LA LEO;

Najua kitu pekee ninachoweza kukidhibiti kwenye maisha yangu ni mawazo yangu. Mimi ndio ninayeweza kuamua nifikirie kitu gani na kitu gani nikipe kipaumbele. Kwa kuweza kudhibiti maisha yangu nitaweza kudhibiti sehemu kubwa ya maisha yangu. Sitakubali mawazo hasi na ya hovyo yatawale akili yangu. Nitaweka mawazo chanya na ya mabadiliko katika akili yangu na nitayafanyia kazi.
 
Uaminifu ni jambo la muhimu sana na wengi wetu tumekuwa wepesi wa kuona wengine si waaminifu kwa kuwa wameenda kinyume na tulivyotegemea iwe. Mfano ni rahisi sasa kusikia wengi wetu tukilalamikia viongozi wanaokosa uaminifu kwa kufanya vitendo visivyofaa au hata kuingia mikataba isiyo na manufaa kwa wengi , ni kweli ni habari mbaya, haifurahishi na inaumiza sana tu katika hali ya kawaida.
 
Lakini tunasahau kuwa hata katika maisha yetu ya kawaida watu wengi wamekosa uaminifu sana, mfano mashuleni na hata vyuoni unakuta watu wengi wanafaulu mitihani yao lakini si kwa njia sahihi, si kwa kufanya kama ipasavyo kufanya ili wafaulu bali njia na mbinu zinazotumika si njema na si sahihi sana machoni pa watu na hata jamii kwa ujumla, lakini kwa kuwa wengi wanafanya hayo na wanaona yakiwafanikisha wanaona ni kitu sahihi tu.
 
Au tuna waalimu ambao hawasahihishi mitihani kwa haki bali wanapewa kitu fulani kidogo ili waweze pindisha matokeo ya mitihani na kwa kuwa labda mtu huyo amekuwa akifanya hivyo kwa muda mrefu anaona ni kitu sahihi au kwa kuwa haijulikani na wengi basi anaona yu sahihi tu.
 
Lakini kuna wanafunzi wenyewe ndio wanaowafuata walimu na kuomba wapewe majibu au namna ya kuweza kufaulu mitihani yao kwa urahisi kwa kuwapa kitu kidogo, na kwa kuwa pengine mtu anakuwa amefanya yeye kama yeye anajua yu salama na sahihi wala hasikii kuhukumiwa ndani mwake na ikitokea amesikia hivyo anapuuzia tu.
 
Maofisini wafanyakazi wengi wamekuwa si waaminifu pia, hasa kwenye swala la muda, wengi wanatumia muda wa kazi kufanya mambo ambayo hayana tija kwa waajiri wao, muda ambao mwajiri anawalipa wao wanafanya mambo ambayo hayamwingizii mwajiri faida, wengine wanachelewa sana kufika ofisini, au wanawahi kutoka kabla ya muda na kwa kuwa labda hakuna mtu anayemfuatilia basi anajiona yuko sahihi kufanya hivi, lakini kuna wengine akisikia tu bosi hayupo siku hiyo basi atachelewa kufika ofisini au atachelewa sana au anaweza wahi kutoka kwa kuwa hakuna mtu wa kumfuatilia au kumuulizwa kwa nini anafanya hivyo.
 
Wengine pia wamekuwa wadanganya waajiri wao kwa kuwapa taarifa zisizo sahihi, mfano mtu ameagizwa akanunue kitu fulani dukani akifika huko ataongeza bei na hata kutengeneze risiti bandia ili tu aweze kuchukua kipato zaidi na kwa kuwa hana mtu wa kuweza kuligundua hilo basi anaona yu salama, wengi wananunua hata vitu visivyo na ubora ilimradi tu aweze kupata kitu kidogo na kufikisha taarifa za uongo kwa mwajiri wake.
 
Imefikia hatua hadi majumbani mwetu uaminifu umekosekana yaani watu wamezoea tabia mbaya mpaka imeonekana ni sahihi, mfano unakuta hata mama pale nyumbani yupo tayari kumdanganya mumewe juu ya matumizi fulani ili mradi tu aweze kutimiza malengo yake , au mwingine anafikia hatua ya hata kuwatesa watu wa nyumbani mwake kwa kuwapa vitu vilivyo chini ya kiwango ili mradi tu aweze kufanya yake, watu wengi wamekosa uaminifu kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…