Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Taarifa kutoka korido za PSG zinaeleza kuwa, Neymar anaonekana kuwa jirani na mlango wa kutokea na kurejea zake Barcelona baada ya uhusiano wa wawili hao kuharibika.

Wakati bifu hilo likizidi kufukuta, vyombo vya habari vya Hispania vinaeleza kuwa, Neymar bado ana kiu ya kuachana na PSG na kurejea Camp Nou kuungana na washkaji zake.
 
Vimekwenda mbali zaidi kwamba, Neymar anataka kutumia kuvunjika kwa uhusiano huo kama kigezo cha kulazimisha kuondoka Paris huku wachambuzi wa mambo wakieleza kwamba, Barca watalazimika kuvunja benki na kulipa pauni 157 milioni ili kumchukua mtu wao huyo, ambaye msimu huu amefunga mabao 16 na asisti 10 kwenye mechi 20 alizocheza.

Uhakika zaidi wa Neymar kuachana na PSG utaongezwa nguvu na vipengele kwenye mkataba wake wa sasa ambao, unamruhusu kununua muda uliobaki kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka Duniani, FIFA. Hata hivyo, kama hilo litatokea basi Neymar atalazimika kupunguza mshahara wake wa sasa hadi 403,000 ili alingane na Messi ambaye ndiye anavuta mzigo mkubwa klabuni hapo.

Wakati mambo yakifichua, kwa upande wake Leonardo amesisistiza kuwa hakuna tatizo na Neymar amekuwa akijitoa kusaidia klabu hiyo.
 
Inaaminika iwapo Spurs ikishindwa kufuzu kushiriki Ligi ya Mabingwa itapunguza bajeti yake ya usajili hadi Pauni 50 milioni, hivyo ili kupandisha bajeti hiyo wanaweza kulazimika kuuza baadhi ya wachezaji mastaa ili kupata pesa ya usajili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…