Watu wanajiuliza wanatakiwa kusubiri hadi lini kabla ya pambano hilo kufanyika. Kilichopo mezani hadi sasa ni kuwa wawili hao watakutana wakati wa kiangazi mwaka huu.
Ilichukua mwaka na zaidi kabla ya Fury na Wilder kurudiana, lakini kwa mujibu wa Arum pambano hilo limepangwa kufanyika Julai 18 (tarehe ya awali) siku chache kabla ya kuanza kwa michezo ya Olimpiki, Tokyo, Japan.
Fury alitawala kila idara katika pambano la kwanza na kumaliza utata wa nani bora kati yao, kwa sababu Wilder alizidiwa mbinu, nguvu, na ubora kwa ujumla.
Kama Fury akishinda tena atamaliza utata wa nani zaidi, kuna uwezekano pambano hili lisiwe na amsha amsha kama lile la pili, lakini bado litakuwa moja kati ya pambano kubwa zaidi kuwahi kufanyika katika miaka ya karibuni.
Kitu kinachofurahisha zaidi kuhusu pambano hili ni kuwa yatasikika mengi sana kuelekea siku yenyewe, kila mmoja atatamba sana kuhakikisha wanavutia watu wengi zaidi katika pambano lenyewe.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.