Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

“Nadhani wapinzani wetu walistahili kuingia nane bora kutokana na kikosi change kusumbuliwa na majeruhi wengi. Hakuna timu ambayo inaweza kukosa wachezaji wake watano hadi sita alafu ikaendelea kufanya vizuri ni lazima wapungue makali,” alisema.
 
FB_IMG_1583923644990.jpeg
 
Uongozi wa Ligi Kuu England (EPL) umeahirisha mchezo baina ya Arsenal na Manchester City uliotarajiwa kuchezwa leo Jumatano usiku kwenye Uwanja wa Etihad jijini Manchester ikiwa ni hatua ya tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi vya corona (Covid-19).
 
Hii ni baada ya taarifa kuwa baadhi ya wachezaji na viongozi wa klabu ya Arsenal wakati wa mechi dhidi ya Olympiacos iliyopigwa siku 13 zilizopita, waligusana na mmiliki wa klabu hiyo kutoka Ugiriki, Evangelos Marinakis ambae amekugundulika na maambukizi ya virusi hivyo hatari hivi karibuni.
 
Kutokana na taarifa hiyo, klabu ya Arsenal imeanza kuchukua hatua mbalimbali za kidaktari ikiwemo kuwachunguza wachezaji na maofisa wa klabu hiyo ambao waligusana na mmiliki huyo, kama ambavyo miongozo ya Serikali ya Uingereza inavyoeleza kwamba, mtu yeyote aliyegusana na mtu mwenye maambukizi ya virusi vya corona, anatakiwa ajitenge nyumbani kwa siku 14 kuanzia siku aliyogusana na mtu mwenye maambukizi.
 
"Kwa hatua zaidi za kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona, tayari tumeshafanya mawasiliano na wageni na wakurugenzi wetu ambao kwa namna moja ama ingine waligusana na wachezaji hivi karibuni, ili kuhakikisha na wao wanachukua hatua za haraka kujitenga, " taarifa kutoka Arsenal anaeleza.
 
Kufuatia kuahirishwa mchezo huo, msimamo wa EPL unaonyesha kwamba, Manchester City inabakia nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 wakati Arsenal iko nafasi ya tisa ikiwa na pointi 40 baada ya klabu zote mbili kucheza jumla ya michezo 28.
 
Back
Top Bottom