Kutokana na taarifa hiyo, klabu ya Arsenal imeanza kuchukua hatua mbalimbali za kidaktari ikiwemo kuwachunguza wachezaji na maofisa wa klabu hiyo ambao waligusana na mmiliki huyo, kama ambavyo miongozo ya Serikali ya Uingereza inavyoeleza kwamba, mtu yeyote aliyegusana na mtu mwenye maambukizi ya virusi vya corona, anatakiwa ajitenge nyumbani kwa siku 14 kuanzia siku aliyogusana na mtu mwenye maambukizi.