Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Kipindi cha vita ya Pili ya Dunia Japan walikuwa na mtindo wa kusababisha milipuko katika maeneo wanayoshambulia kwa marubani kujitoa mhanga kwa eneo husika, walikuwa wanaitwa Kamikaze. Kuna Rubani aliuwawa kwa kupigwa risasi na maofisa wa ngazi za juu jeshini baada ya kudai amekosa eneo la kujitoa mhanga zaidi ya mara 9.
 
Popo' ana uwezo wa kuwasiliana na Popo wenzake kwa mmoja mmoja (One to one communication) kwa kuwasilisha taarifa tofauti kama binadamu ambavyo anaweza kuwasiliana na watu tofauti tofauti kwa kuwasilisha taarifa tofauti pia. Wanyama wengi hawana uwezo huo
 
Nyani wanatumiwa kuvuna nazi nchini Thailand, Sri Lanka, Malaysia, Indonesia na India. Nyani hufundishwa kufanya kazi hiyo na wataalamu wa kilimo na wanyama. Kwa wastani ndani ya siku, nyani wa kiume anavuna nazi 1600, wa kike 600 na binadamu anavuna 80. (NPR)
 
Tembo ana uwezo wa kutafuna majani ya dawa kuanzisha uchungu wa kuzaa, kutambua vitu kwenye kioo, kuigiza sauti mbalimbali na kutumia vitu mbalimbali kwa matumizi sahihi pasipo kufundishwa. Pia ndiyo wanyama pekee wanaoweka msiba pale mwenzao anapokufa. (World Atlas)
 
NjiwaAna uwezo wa kutambua herufi zote 26, ana uwezo wa kurudi nyumbani hata akiwa kilomita mamia kutoka nyumbani na ndiyo sababu walikuwa wanatumika kutuma ujumbe. Wauza madawa ya kulevya pia wanawatumia kuuza madawa hasa magerezani.
 
Wakorea wengi hawatumii pafyumu kwa sababu hawatoi harufu kwapani. Watu wa jamii ya Korea na baadhi ya nchi zingine (Asia mashariki na Amerika kusini) wana jini (gene) ya ABCC11 ambayo inazuia utengenezwaji wa vitu vinavyogandisha jasho mwilini na kusababisha harufu mbaya. Ni vigumu kupata pafyumu kwenye maduka ya Korea. (News-medical)
 
Back
Top Bottom