Elysia chlorotica ndiyo mnyama pekee anayeweza kujitengenezea chakula chake mwenyewe kama mmea. Mnyama huyo anayepatikana kwenye bahati ya Atlantic ana chembeumbijani (chroloplasts) anazozipata kwa kula mimea na kisha anazitumia kujitengenezea chakula. (National Geographic)
Tanzania: Vifo vinavyotokea kwa vijana kati ya umri wa miaka 19-29 "kujiua" inachukua nafasi ya pili huku ya kwanza ikiwa ni ajali. Vijana wa "kiume" ndio wanaongoza kwa kujiua zaidi kuliko wa kike.
Nchini Japan, Valentine's day ni siku ambayo wanawake wanatakiwa kuwapa zawadi wanaume. Mwezi mmoja baadae wanaadhimisha White day ambapo wanaume wanawapa wanawake zawadi. (BBC)
Nyangumi wa bluu ndiye mnyama mkubwa na mzito kuliko wote duniani. Ana uzito wa kilo 201,000 (tani 210) na zaidi. Uzito wa ulimi wa nyangumi ni sawa na uzito wa tembo mmoja.
Nyangumi wa bluu ndiye mnyama mkubwa na mzito kuliko wote duniani. Ana uzito wa kilo 201,000 (tani 210) na zaidi. Uzito wa ulimi wa nyangumi ni sawa na uzito wa tembo mmoja.
Pweza ndiye mnyama pekee wa baharini mpaka sasa mwenye uwezo wa kuiga aina mbalimbali za wanyama. Pweza huweza kuiga aina 15 za viumbe wengine wa baharini mfano: rangi,uogeleaji,umbo,kasi n.k
Umri ambao mtu anaanza kufanya mapenzi unaweza kusababishwa na vinasaba alivyorithi kutoka kwa wazazi wake. 25% ya watu hufanya ngono kwa mara ya kwanza katika umri sawa na ambao ndugu zao wengine walianza. (TheGuardian)
Nzi dume hupatwa na stress kama akikataliwa na jike kujamiiana. Utafiti unaonesha huwa na kawaida ya kunywa pombe ili kuondoa stress baada ya kukataliwa.
Mvi' hutokea baada ya seli zinazotengeneza rangi ya nywele kuchoka au kufa. Kupata mvi katika umri mdogo huitwa "Canities" hutokana na muingiliano wa jini (gene) za urithi, mazingira na lishe.
Simu ya kwanza ilitengenezwa na Alexander Graham Bell mwaka 1876. Mpaka anafariki alikataa kabisa kutumia simu sababu akitaja ni kuweka umakini zaidi katika kazi zake, hivyo kutumia simu ingemchanganya
Saikolojia: Kukosekana kwa malumbano' mara kwa mara katika mahusiano ni mojawapo ya kiashiria kuwa upendo umepungua baina yenu. Watu wanaopendana huwa na kawaida ya kulumbana na kukorofishana mara kwa mara.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.