Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Margaret Thatcher' ndiye mwanamke wa kwanza kuwa Waziri Mkuu nchini Uingereza kutoka 1979-1990. Lakini pia ndiye Waziri Mkuu pekee aliyekuwa na Digrii ya Sayansi, alikuwa na digrii ya Kemia. Mpaka sasa hakuna Waziri Mkuu mwingine aliyetokea kuwa na Digrii ya Sayansi.
 
Hakuna utafiti wowote unaothibitisha kuwa matumizi ya Bangi huathiri ukuaji wa seli za ubongo. Baadhi ya tafiti zinaonesha matumizi ya Bangi huongeza ukuaji zaidi wa seli za ubongo.
Vyanzo: Heathline, Webmd, MIT..
 
Anti- Natalism ni mtizamo ambao watu mbalimbali huamini kuwa binadamu hatakiwi kuzaa. Anti-Natalists wanapinga binadamu kuwa na watoto na mojawapo ya sababu wanayotoa ni kwamba watoto hawajaweka wazi kama wanataka kuzaliwa hivyo kuzaa ni kukiuka haki zao.
Chanzo: BBC
 
Filamu ya Saw' ilishutiwa kwa siku 18 tu na sehemu kubwa ilikuwa katika eneo moja. Kutoka bajeti ya $1.2 M ilifanikiwa kuuza zaidi ya $103.9M na kuwa filamu nyingine ya kutisha iliyopata faida zaidi tangu itoke Scream (1996).
 
Marekani haina lugha rasmi ya taifa, hakuna sababu yoyote ambayo imetajwa katika Katiba lakini inasemekana ni kutokana kwa uwepo wa lugha mbalimbali zinazotumika katika majimbo mbalimbali japo kiingereza ndiyo hutumiwa zaidi.
Chanzo: World Atlas
 
Nchini Korea Kaskazini kuna madini mbalimbali yenye thamani ya dola trilioni 6-10 hayajachimbwa bado. Sababu kuu ni nchi hiyo kutokuwekeza kwenye teknolojia na wataalamu wa kuchimba madini hayo. Korea ya Kaskazini ni moja ya nchi ambazo zina bajeti ndogo duniani (TZS Trilioni 40 kwa mwaka) na umasikini kwa wananchi ni wa kiwango kikubwa. (BusinessInsider)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…