Kiangazi mwaka jana, Joao Felix aliingia kwenye historia ya kuwa mchezaji kinda aliyesajiliwa kwa mkubwa mrefu zaidi, baada ya Atletico Madrid kuvunja benki kumsajili. Baada ya kuanza vizuri maisha yake ndani ya Atletico katikati hapa alitetereka, lakini bado anaonekana kuwa ni moto wa kuotea mbali.
Kwanza tambua hili Mbappe si mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi Paris Saint Germain pekee bali jamaa ndiye mchezaji mwenye thamani kubwa katika klabu zote za ligi tano kubwa za Ulaya.
Rashford msimu huu amezidi kukuza jina lake kutokana na kuanza msimu na moto hadi alipopata majeraha. Thamani yake kwa kiasi kikubwa imechangia sana kupandisha thamani ya kikosi cha Man United kwa ujumla.
Inashangaza kuona Tammy Abraham, sasa ana thamani ya zaidi ya Euro 100 milioni, wakati msimu ulipita tu alikuwa Ligi Daraja la Kwanza katika kikosi cha Aston Villa kwa mkopo. Fomu yake mbele ya lango ndiyo kwa kiasi kikubwa imepandisha thamani yake.
Mchezaji anayeshika nafasi ya pili ni zao lingine la Chelsea, Mason Mount kwa upande wake thamani yake ni Euro 94.1 milioni.
Inashangaza kidogo kuona Real Madrid yenye utamaduni wa kujenga vikosi vya mastaa tupu mchezaji wake mwenye thamani zaidi anakuwa na thamani ya Euro 90.3 milioni.
Hazard thamani yake inaweza kupanda zaidi kama tatizo la majeraha ya mara kwa mara litamuisha maana hilo ndilo limemshusha.
Licha ya kuelekea mwisho wa maisha yake ya soka Messi bado ndiye mchezaji mwenye thamani zaidi pale Barcelona. Mshindi mara sita wa tuzo ya Ballon d’Or ndiye mfalme katika kikosi cha miamba hiyo ya Nou Camp.
Wakati huu ambao Messi anazidi kuzeeka kuna kila dalili kuwa Antoine Griezmann (Euro 123.6 milioni) ndiye atakuja kuvaa viatu vyake.
Kama klabu yake, Sterling naye msimu huu kiwango chake kimekuwa kikipanda na kushuka, lakini bado ndiye mchezaji mwenye thamani kubwa zaidi katika kikosi cha Manchester City.
Gabriel Jesus (Euro 115.6 milioni) ndiye anamfuata kwa karibu zaidi Sterling katika kikosi cha Man City.
Hakuna cha kushangaza hapa, japokuwa Mo Salah amemzidi kidogo tu Sadio Mane (Euro 155.6 milioni). Akiwa na mabao 91 katika mechi 144 tangu arudi England itahitaji dau la kufa mtu kumng’oa staa huyo wa Kimataifa wa Misri pale Anfield.
Liverpool ina wachezaji wengi wenye thamani kubwa mfano Alisson Becker (Euro 87 milioni), Virgil van Dijk (Euro 93 milioni) na Trent Alexander-Arnold (Euro 110 milioni).
KUNA wachezaji ukitazama takwimu zao kwenye kucheka na nyavu unakubali kuwa wao ni hatari, lakini huwezi kuamini kuwa wengi kati yao pia ndio wanaongoza kwa kukosa mabao ya wazi.
Hivi umewahi kukaa na kujiuliza ni mchezaji gani anaongoza kwa kukosa mabao kwenye ligi tano kubwa barani Ulaya? Kama hilo swali limewahi kupita kwenye akili yako basi jibu lake liko hapa.
Kuna wachezaji wamekuwa wakipondwa sana katika kipengele hicho cha kukosa mabao ya wazi na zile kauli za “angekuwa fulani pale hakuachi” wachezaji kama kina Romelu Lukaku, Anthony Martial, Olivier Giroud na Alexandre Lacazette lawama hizi kwao ni kawaida tu.
Lakini, huwezi kuamini unapozungumzia wachezaji wanaokosa sana mabao katika ligi kubwa tano za Ulaya majina hayo huwezi kukutana nayo, badala yake utakutana na yale makubwa ambayo ni ndoto ya kila mtu kuona yanaongoza vikosi vyao.