Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Thomas de Mahy, alikuwa anaunga mkono utawala wa Ufaransa uliotolewa madarakani kwa mapinduzi karne ya 18. Baada ya mapinduzi alihukumiwa kunyongwa. Alipopewa karatasi ya hukumu asaini, alisoma kisha akamwambia hakimu "Kuna maneno matatu mmekosea kuandika". (Wikipedia & VintangeNews)
 
Amado Carrillo Fuentes maarufu kama "Lord of the Skies" alipewa jina hilo sababu alikuwa anamiliki Ndege tofauti 727 alizokuwa anatumia kusafirisha madawa ya kulevya. Alikuwa akifanya Upasuaji mara kwa mara kujibadilisha viungo mbalimbali kama sura ili kuwakwepa polisi. Alifariki mwaka 1997 sababu ikiwa kuzidisha sana Upasuaji wa mwili wake.
 
Wakati wa vita kuu ya kwanza ya dunia, mbwa mwitu wenye njaa walivamia makambi ya wanajeshi wa Urusi na Ujerumani na kuanza kuwala. Ilibidi wanajeshi hao (ambao walikuwa maadui) waungane kwa muda kupambana na mbwa mwitu kwanza.
(War History)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…