Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Sisimizi wafanyakazi baadhi huenda kutafuta chakula ambapo wakiwa njiani huacha kemikali katika njia zote ambazo watapita mpaka waone msosi. Wakifika katika msosi wanaotaka hutoa kemikali nyingi zaidi ambazo huwataarifu waliobaki nyumbani ambao huanza kufuata kemikali kupitia njia zilizotolewa na wenzao. Na wakati wa kurudi hufuata kemikali hizo.
 
Kwenye Ubongo kuna Mabilioni ya Seli ambazo zimevunjika vunjika ambapo ili kuwasiliana pamoja ndipo hutumia hizo Kemikali ili kuungana....Baadhi ya kemikali Zinazofahamika sana ni Dopamine, Serotonin, acetylinelcholine, Noradrenaline etc.
 
Madawa ya kulevya, Hususani 'Unga'...Huleta madhara makubwa katika Ubongo..Madawa huaribu Neurotransmitters....hizi ni kemikali zinazotolewa na ubongo ambazo husaidia katika kuhakikisha safari ya neva za seli kutoka moja kwenda nyingine inafanyika ipasavyo.
 
Kazi ya 'dopamine' (Kukupa raha), noradrenaline (Kupambana) and 'serotonin' (Mood)....Sasa unapotumia madawa ya kulevya Unaaribu Neurotransmitters, hali inayoweza kupelekea kuongezeka au Kupungua kwa uzalishaji wake...ndio maana Kuna watu wakitumia Madawa tu, Unakuta anakuwa mgomvi tofauti na akiwa kawaida hajatumia
 
Sasa kwa ndugu zetu wanaoutumia Unga hawa ndio balaa zaidi, Sehemu kubwa inayoathirika ni Kemikali hii ya Dopamine...ambayo kazi yake ni kukupa ile raha ambayo huwezi mwelezea mtu 😊😊 mfano kama Mwanaume anapopiga bao (Kufikia kilele) kuna raha fulani inadumu kama sekunde 10 hivii....Sasa unaambiwa Ukitumia 'Unga' ile raha ile, ile raha inaweza kudumu kwa takribani Mpaka dakika 30...hadi Saa nzima.
 
Kitu kibaya ni wanapoanza, huanza mdogo mdogo, lakini baadae huzidisha zaidi kiasi kwamba Ubongo unakufa kabisa kuzalisha kemikali hizo...hivyo Bila Unga kwako inakuwa tabu...sababu mwili unakuwa unahitaji ili kuuweka Sawa...hapo ndipo tunasema mtu amekuwa adicted
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…