Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Yesu zamani Bethlehem
Aliyezaliwa kwa aibu
Ndiye mwokozi wa ulimwengu
Akaja kwa Mimi


Yesu akafa msalabani
Kuniponya akalipa Deni
Ni ajabu ya jinsi gani
Kunifia Mimi

Ni yeye Huyo Tangu Asili
Na nilipotangatanga mbali
Alikuja kwa upole kweli
Kuniita Mimi

Yesu kristo atarudi Tena
Hilo lanifurahisha Sana
Yeye bwana akionekana
Kunijia mimi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jina lake Yesu tamu
Tukilisikia
Hutupoza tena hamu
Hutuondolea
/Hutuondolea

Roho iliyoumia
Kwalo hutibika
Chakula njaani pia
Raha tukichoka
/Raha tukichoka

Jina Hili Ni msingi
Ngao,ngome mwanga
Kwa hili napata wingi
Kwangu Ni akiba
/Kwangu Ni akiba

Yesu mchunga,rafiki,
Mwalimu,kuhani,
Mwanzo,mwisho,njia,Haki,
Uzima kifoni
/Uzima kifoni

Moyo wangu hauwezi kukusifu kweli
Ila sifa zangu hizi
Bwana zikubali
/Bwana zikubali

Na utakaponiita
Kuja kwako Bwana
Huko kwako sitaacha
Kukusifu kweli
/Kukusifu kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji849][emoji849]Kuna habari gani kwani mtani??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…