Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Usitumie kilevi/pombe

Kama nilivyoeleza katika hoja ya kwanza, “melatonin” ni homoni muhimu inayotuwezesha kulala. Utafiti uliofanyika umebaini kuwa uzalishaji wa homoni hii huathiriwa sana na matumizi ya pombe.Pombe ni kinywaji ambacho kimeonyesha kuwa na hasara nyingi katika mwili wa binadamu, hivyo ni vyema ukajitahidi kuepuka matumizi ya pombe.
 
Boresha mazingira ya chumba unacholalaUtafiti unaonyesha kuwa zaidi ya asilimia 50 ya watu wanaopata matatizo ya kulala yanasababishwa na mazingira mabaya ya vyumba vyao vya kulala. Hakikisha unalala kwenye chumba ambacho hakina mwanga mwingi, joto kali, baridi, uhaba wa hewa au kelele.
 
Mambo unayoweza kufanya ili kuboresha chumba chako:Zima au punguza mwanga katika chumba chako.Zima redio, televisheni au kifaa kingine kinachosababisha kelele.Fungua madirisha ili kuhakikisha unapata hewa yakutosha.Tawala joto na baridi kwani visipokuwa vya wastani hutoweza kulala vyema – angalau nyuzi joto 20 zinatosha.Naamini ukizingatia haya utaboresha chumba chako na kukuwezesha kulala vyema.
 
Usile sana usiku au usile vyakula vizito usiku

Kutokana na watu wengi kuwa na shughuli nyingi wakati wa mchana hushindwa kula vyema mchana; hivyo wanapendelea kula sana usiku.

Hili si jambo zuri kwani mwili unakuwa umepumzika wakati wa usiku; hivyo kula sana au kula vyakula vigumu kutapelekea mwili kutumia nguvu kubwa kumeng’enya chakula hicho. Ndiyo maana watu wengi wanaopendelea kula sana usiku huamka asubuhi wakiwa wamechoka sana.
 
Pumzisha na safi akili yako jioni

Kuna umuhimu wa kusoma au kusikiliza vitu vyenye kuburudisha na kuliwaza akili yako jioni kwani kutafanya akili yako kukuruhusu kupata usingizi wa uhakika.

Mambo ya kufanya katika hoja hii:

Epuka kutazama au kusikiliza filamu (Movies) au masimulizi ya kutisha (Hili litakuondolea maruweruwe na mang’amung’amu usiku).
 
Oga jioni au kabla ya kulala

Utafiti uliofanyika umebaini kuwa, kuoga jioni au usiku kabla ya kulala, kutauweka mwili wako katika hali nzuri kiafya na kukufanya kulala vyema. Hivyo unaweza kuoga kabla ya kulala ua hata kusafisha miguu yako kwa maji kabla ya kulala ili kukuwezesha kupata usingizi mzuri.
 
Tumia godoro na mto bora

Watu wengi hujiuliza ni kwa nini huwa wanalala vyema kwenye hoteli kuliko nyumbani kwao. Jibu ni kutokana na kutumia godoro na mto bora zaidi kuliko ule wanaoutumia nyumbani kila siku.

Godoro duni na mto duni vitakusababishia maumivu ya shingo na ya uti wa mgongo hivyo kusababisha usilale vyema. Jitahidi kuhakikisha unanunua na kutumia godoro na mto ulioidhinishwa na wataalamu.
 
Fanya mazoezi; lakini si kabla ya kulala

Mazoezi ni muhimu kwa ajili ya kujenga na kulinda afya ya mwili wako. Jitahidi kuwa mtu anayefanya mazoezi mara kwa mara kwani kutakuongezea uwezo wa kulala vyema wakati wa usiku; kwa kuwa mwili utajipumzisha vyema ili kujijenga tena.
 
Usinywe vimiminika kwa wingi usiku

Maji ni muhimi kwa ajili ya afya yako, lakini unywaji wa maji mengi au vimiminika wakati wa usiku si jambo jema kiafya. Kunywa maji au vimiminika kwa wingi usiku kutakusababisha kuamka mara kwa mara kwenda uwani; hivyo utakuwa na usingizi unaokatishwa katishwa mara kwa mara.

Ni vyema kujijengea mazoea ya kunywa maji au vimiminika kidogo usiku au ikibidi kunywa kwa wingi basi vinyweke mapema.
 
Nionapo amani Kama shwari
Ama nionapo shida
Kwa mambo yote umenijulisha
Ni Salama rohoni mwangu

/Salama rohoni
Ni Salama rohoni mwangu

Ingawa shetani atanitesa
Nitajipa moyo kwani
Kristo ameona unyonge wangu
Amekufa kwa roho yangu


Dhambi zangu zote Wala SI nusu
Zimewekwa msalabani
Wala sichukui laana Yake
Ni Salama rohoni mwangu

Eh Bwana himiza siku ya kuja
Panda itakaapo Lia
Utakaposhuka sitaogopa
Ni Salama rohoni mwangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwamba wenye imara
Kwako nitajificha
Maji hayo na damu
Yaliyotoka humu
Hunisafi na dhambi
Hunifanya mshindi

Kwa kazi zote pia
Sitimizi Sharia
Nijapofanya bidii
Nikilia na kutii
Hayaishi makosa
Ndiwe wa kuokoa

Sina Cha mkononi
Naja msalabani
Nili mtupu nivike
Ni mnyonge nishike
Nili mchafu naja
Nioshe nisijafa

Nikungojapo chini
Na kwenda kaburini
Nipaapo mbinguni
Na kukuona enzini
Roho yangu na iwe
Rahani mwako Wewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…