Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Yani mtu anakufa huku unamuona
Ni moja ya maumivu makali sana anayo baki nayo mshuhudiaji.
Nakumbuka kwenye harakati zangu za kutafuta pa kutokea ujanani tukiwa tumetoka Mocimboa da praia port tupo uelekeo wa rasi ya Palma tukiwa kwenye boti, tuliwapita Wamakua 26 kwenye chombo cha kutweka/mashua ( Daemusin anakijua vizuri) wakiwa wamejaza mahindi wanayapeleka Mtwara kuyauza. Saa 11 alfajiri taa za visiwa vya Commoro zikiwa zinaonekana kwa kufifia kudhihirisha kumekucha tukawa tunakatisha mto Ruvuma, Wamakua tulikuwa tumeachana nao kama mita 40 hivi, sheria za kuuvuka mto unaotembea ni kwa kuukata angle si zaidi ya nyuzi 30,ni eidha uufuate au uukimbie kwa nyuzi 30.

Hata sijui nini kiliwachanganya, maana pomboo walikuwepo wengi sana kama waongoza njia, yaani ndani ya dakika chombo kikawa kimepinduka na hakuna hata mtu anaonekana kuomba msaada.
Ndio, wote 26 wakaishia pale, ni mkondo mkali sana pale, hatukuona mtu. Walikufa maji.
Miaka24 imepita sijawahi kusahau, harakati zangu za kupita kwenye maji zikaishia hapo.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inasikitisha sana
 
ngoja hii hadithi yako niisome tena kwa mara ya 10 huenda nitaielewa.
code za kibabe

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…