Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Jo-Anne-Lungile-1024x1024.jpg
 
Mwenyezi Mungu mtukufu amponye kijana huyu wa kidachi ili arejee uwanjani
amen,
kwa sisi tunao amini uwepo wa Mungu kitendo cha huyo bwana mdogo kuwa katika hali ya kupoteza fahamu kwa takribani miezi 33 na baadae kurudi tena ni zaidi ya muujiza wa kuthibitisha nguvu ya Mungu ya kutokushindwa.

1585306095271.png
 
Ameandika Janet Otieno muimbaji nyimbo za Injili kutoka nchini Kenya.
______________________
Wapendwa wanaume,
Muda mwingine Mimi hujiuliza mnatoa wapi hizi nguvu. Kwa miezi unakaa bila hata kujinunulia mwenyewe nguo yoyote ili tu ulete chakula mezani (nyumbani). Unashinda njaa ili familia yako ipate chakula iweze kuishi. Unaamka unavaa na kuondoka nyumbani bila hata kujua unaenda wapi lakini unarudi nyumbani na pesa baada ya mihangaiko.

Iwe mchana au usiku wengi wenu mmekuwa mkiaibishwa, kudharauliwa na kunyanyaswa kwa ajili ya kuzitafutia riziki familia zenu. Baadhi yenu hamjaweza kupata kazi zenye heshima na unapopeleka "karanga" nyumbani wanakurushia usoni.

Najua mmekuwa mkijinyima ili watoto wenu wapate chakula, nguo, malazi na elimu. Mara nyingine mmetukanwa na kunyanyaswa na watu mliowazidi umri lakini mmeyachukua maumivu yote kwa ajili ya wake zenu, watoto, na wazazi wenu wanaowategemea.hata pale unapofika nyumbani upumzike unamkuta mke kanuna bila sababu huku akionesha madharau makubwa lkn bado huwa hamkati tamaa,

Mara nyingine haijalishi kama una kazi ama lah, umepata au umekosa, unatakiwa uitunze familia. Hilo ni jukumu lako kama mwanaume.

Unalipa mahari kubwa ili umuoe mwanamke unayempenda na mara nyingine unajikuta unaitunza familia yake, kwa sababu ndugu zake ni ndugu zako pia.ili mke akuheshimu lk unajikuta unaambulia madharau tupu,

Mnawezaje kufanya hayo yote ya kushangaza? Ninawaombea BWANA Mungu abariki juhudi zenu. Jasho lenu lisiwe bure. Muendelee kuishi kwenye mioyo ya mama zenu, wake zenu, watoto wenu na wote muwapendao katika Kristo.

Nawaombea Mungu aendelee kuwabariki kwa upendo wenu usio na kipimo na dhabihu mnazotoa kwa ajili ya familia zenu. Amen.!
 
ahsante kwa tafsiri safii ya kiswahili.
niliisoma kwa kiingilishi nikadhani alikuwa anawadhihaki wanaume (kumbe alikuwa anawasifia na kuonyesha shukurani zake kwa jinsia ya kiume)

itabidi nikajifunze kiingilishi kwa lazima
 
Back
Top Bottom