Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

David Ginola,kiungo

David Ginola alishinda tuzo ya Mchezaji Bor wa Mwaka kwenye Ligi Kuu England msimu wa 1998/99. Msimu huo ndio ambao Manchester United ilishinda mataji matatu makubwa, lakini kiungo wa pembeni wa Tottenham Hotspur, Ginola ndiye aliyechaguliwa kuwa bora. Ginola alitua England kwa mara ya kwanza aliposajiliwa na Newcastle United ya kocha Kevin Keegan mwaka 1995 na aliichezea pia Aston Villa na Everton kabla ya kustaafu soka.
 
N’Golo Kante,kiungo

N’Golo Kante alikuwa mchezaji wa kwanza wa ndani kushinda mataji ya Ligi Kuu England kwa misimu miwili mfululizo kupitia klabu mbili tofauti, alipobeba akiwa na Leicester City na Chelsea katika misimu ya 2015/16 na 2016/17 mtawalia. Alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kwenye Ligi Kuu England akiwa Chelsea baada ya kuisaidia kubeba ubingwa. Kante alikuwa hafahamiki kabla ya majira ya kiangazi mwaka 2015 wakati Leicester City ilipomnasa kwa Pauni 5.6 milioni kutoka Caen. Ni moja ya viungo bora kabisa kuwahi kutokea kwenye Ligi Kuu England.
 
Claude Makelele,kiungo

Real Madrid walikuwa kwenye wakati mgumu katikati ya miaka 2000 wakati ilipoamua kumpiga bei Claude Makelele na kushindwa kusajili mbadala wake. Chelsea walimsajili mchezaji huyo na kwenda kuonyesha kiwango bora kabisa katika Ligi Kuu England. Uwezo wake mkubwa wa kukaba uliwafanya mashabiki na wachambuzi kuitambua nafasi yake anayocheza ndani ya uwanja kama nafasi muhimu. Makelele hakuwa mfungaji, isipokuwa alikuwa ukuta imara wa kuzuia timu isifungwe.
 
Patrick Vieira,kiungo

Patrick Vieira daima atakumbukwa kama mmoja wa wachezaji wa kigeni waliowahi kucheza kwenye Ligi Kuu England. Alishinda mataji mawilimawili makubwa mara mbili tofauti akiwa na kikosi hicho, huku alikuwa nahodha kwenye kikosi cha Arsenal kilichocheza kwa msimu mzima bila ya kupoteza, 2003/04. Alikuwa na upinzani mkali na kiungo wa ManchesterUnited, Roy Keane. Vieira aliwasili Arenal mwaka 1996. Licha ya kwamba hakuwa amesajiliwa na kocha Arsene Wenger, ambaye alijiunga na timu hiyo miezi michache badaye, alifanikiwa kuwa mmoja wa wachezaji bora chini ya kocha huyo Mfaransa.
 
Robert Pires, kiungo

Robert Pires alikuwa Mfaransa mwingine aliyetikisa kwenye Ligi Kuu England akiwa chini ya Arsene Wenger, akishinda tuzo ya mchezaji bor wa mwaka kwenye Ligi Kuu England msimu wa 2001/02 wakati alipoisaidia Arsenal kubeba mataji mawili, Ligi Kuu England na Kombe la FA. Pires alifahamika vyema kwa uwezo wake wa kuuchezea mpira na kuonyesha soka la mvuto hasa katika msimu wa 2003/04, ambapo alifunga mabao 14 akishambulia kutokea kwenye kiungo ya pembeni.
 
Eric Cantona,mshambuliaji

Eric Cantona alikuwa homa ya jiji wakati alipokuwa akikipiga Manchester United, ambapo aliifanya timu hiyo kutawala Ligi Kuu England katikati mwa miaka ya 1990. Alifunga mabao muhimu katika misimu wa 1992/93, 1993/94 na 1995/96 kuisaidia timu hiyo kushinda mataji na alikuwa moto katika kubeba makombe mengine. Cantona alikuwa nahodha wa Old Trafford na kwenye kikosi hicho amefanikiwa kuweka alama zake za kudumu na kuheshimika kama gwiji wa klabu hiyo yenye historia pana kwenye Ligi Kuu England.
 
Thierry Henry, mshambuliaji

Hakuna ubishi kwamba Thierry Henry ni moja ya wachezaji bora kabisa kuwahi kutokea kwenye Ligi Kuu England. Staa huyo ni mfungaji wa mabao wa muda wote katika kikosi cha Chelsea baada ya kufunga 228. Henry anashikilia pia rekodi ya kuwa mchezaji aliyeshinda Kiatu cha Dhahabu mara nyingi, akifanya hivyo mara nne. Awali alikuwa akicheza kama winga kabla ya kocha Arsene Wenger kumbadili na kumtumia kama mshambuliaji wa kati, eneo ambalo alilitendea haki kwa kufunga mabao kama alivyotaka. Alikuwa balaa.
 
Kwa mfano, Xavi na Iniesta. Rio Ferdinand na Nemanja Vidic. Emery Heskey na Michael Owen. Hiyo ni kwa kuwataja kwa uchache tu, kwamba walikuwa na muunganiko mzuri walipokuwa wakicheza timu moja kwenye mchezo wa soka.
 
Kwahiyo ina maana ule ugomvi wake na yule bwana furani utakuwa umemfikisha mahali pabaya kiasi hicho!!?
Hope yupo mahali salama anakula anavyovipenda.
Tujue tu kuna maisha mbali jf
 
One of the greatest player ever in passing,dribbling, shooting and acceleration.....
niliwahi kumshuhudia akicheza soka.
kipindi hicho nina miaka 40 ya kuzaliwa
 
Trump Korona imemchanganya anatukana kila mtu isipokuwa yeye mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…