Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Uzi maalum wa kupeana Likes: Comment chochote upate "Like"

Usiku wa ndizi[emoji2089][emoji2089]
FB_IMG_1585967631349.jpeg
 
Hugo Lloris, kipa

Kipa Hugo Lloris amekuwa akitamba kwenye Ligi Kuu England kwa karibu miaka 10 sasa tangu aliponaswa na Tottenham Hotspur kutokea Lyon kwa ada ya Pauni 8 milioni.

Pia ndiye nahodha wa timu ya taifa ya Ufaransa na Spurs, alipokabidhiwa kitambaa hicho jumla mwaka 2015. Kama ilivyo kwa makipa wengine, wakati mwingine Lloris kiwango chake kinakuwa kinashuka, lakini hilo halimfanyi kuondoka kwenye orodha ya makipa mahiri kabisa waliowahi kutokea kwenye ligi hiyo, tena akicheza timu ya Big Six.
 
Aymeric Laporte,beki

Hana muda mrefu sana tangu alipotua kwenye Ligi Kuu England, lakini hakuna ubishi, Aymeric Laporte ni moja ya wachezaji mahiri wa Ufaransa waliowahi kucheza kwenye Ligi Kuu England. Laporte tayari ameshabeba mataji mawili ya Ligi Kuu England tangu alipojiunga na Manchester City na jambo hilo pamoja na ubora wake linampa nafasi katika kikosi hiki. Pengo la Laporte limeonekana wazi msimu huu kwenye kikosi cha Man City na kuwafanya waruhusu mabao ya kizembe yaliyowagharimu na kuachwa pointi 25 na Liverpool kwenye msimamo wa ligi.
 
Marcel Desailly,beki

Marcel Desailly alitokea kubeba ubingwa wa Kombe la Dunia 1998 wakati alipojiunga na Chelsea, huku kabla ya hapo alitokea kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na vikosi vya Marseille na AC Milan. Kwa kipindi hicho alihesabika kama mmoja wa mabeki bora duniani. Beki huyo, Desailly aliifanya Chelsea kuwa moja ya timu bora kwenye Ligi Kuu England tena kabla hata ya klabu hiyo kuanza kuwa chini ya umiliki wa bilionea wa Russia, Roman Abramovich. Ni bonge la beki kutoka Ufaransa aliyewahi kukipiga Ligi Kuu England.
 
Patrice Evra,beki

Patrice Evra alitokea benchi katika mechi yake ya kwanza kwenye kikosi cha Manchester United na alipata shida kidogo kuhimili mipira ya juu kwenye mchezo dhidi ya Manchester City. Lakini, baadaye beki huyo Mfaransa alituliza daluga zake kwenye Ligi Kuu England na kucheza soka la kiwango cha juu akipata heshima ya ugwiji kwenye kikosi cha Man United, ambapo alikabidhiwa kitambaa cha unahodha. Man United ilinasa huduma ya beki huyo kwa ada ya Pauni 5.5 milioni Januari 2006 na hadi mwaka 2014, Evra alishinda mataji 10 makubwa, ikiwamo Ligi ya Mabingwa Ulaya na mataji matano ya Ligi Kuu England.
 
David Ginola,kiungo

David Ginola alishinda tuzo ya Mchezaji Bor wa Mwaka kwenye Ligi Kuu England msimu wa 1998/99. Msimu huo ndio ambao Manchester United ilishinda mataji matatu makubwa, lakini kiungo wa pembeni wa Tottenham Hotspur, Ginola ndiye aliyechaguliwa kuwa bora. Ginola alitua England kwa mara ya kwanza aliposajiliwa na Newcastle United ya kocha Kevin Keegan mwaka 1995 na aliichezea pia Aston Villa na Everton kabla ya kustaafu soka.
 
Nauliza ni yupi anashambuliwa kati ya Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dr.Tedros, WHO yenyewe, Nchi ya China au wote kwa pamoja?, tuweke nguvu katika kupambana na corona, hizi siasa nyingi kiukweli Afrika hatuzitaki, kwanza ni nani anazitaka?, sisi Afrika tunasimama na Dr.Tedros”- KAGAME
 
Back
Top Bottom